WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kukutana na wafanyabiashara wa soko la
Sabasaba mkoani Dodoma ili kuzungumzia namna ya kulikarabati na
kulifanya liwe la kisasa.
Amesema
miongoni mwa mambo watakayoyajadili katika kikao hicho ambacho hakutaja
siku ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara hasa kwa
wanaouza bidhaa nje ya maduka.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2016) wakati
alipotembelea maduka hayo yaliyoko katika barabara ya One Way inayopita
katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la Sabasaba akiwa
kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.
Amesema
Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo wafanyabiashara wanatakiwa
kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili waweze kumudu
ushindani wa soko.
“Wafanyabiashara
lazima mboreshe biashara zenu, muongeze usafi zaidi na ikiwezekana
muimarishe majengo yenu yawe ya kisasa zaidi kwani haiwezekani maduka ya
Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali hii,” amesema.
Pia
Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara hao wasiogope kwenda kukopa katika
taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kujiongeza mitaji na
kupanua biashara.
Amesema
tayari alishatoa maagizo kwa wamiliki wa benki kuhakikisha
wanawawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo, hivyo aliwataka
wasiogope na badala yake wachangamkie fursa hiyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea Mtaa wa One Way mjini Dodoma Oktoba 5, 2016.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea eneo maarufu la biashara mjini Dodoma
la Sabasaba Oktoba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na baadhi ya viongozi wa soko hilo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia moja ya nguo ya mtumba alipotembelea soko hilo la Sabasaba Mkoani Dodoma Oktoba 5, 2016.
No comments:
Post a Comment