Na MatukiodaimaBlog
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ametoa muda wa miezi sita kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha shule zote 52 za Msingi katika Manispaa ya Iringa zinakuwa na vyoo bora vinginevyo shule itakayobainika haina choo bora itafungwa
MKUU wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela ametoa muda wa miezi sita kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha shule zote 52 za Msingi katika Manispaa ya Iringa zinakuwa na vyoo bora vinginevyo shule itakayobainika haina choo bora itafungwa
Pamoja na kutoa agizo hilo kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa pia amewaagiza watendaji wa kata na mitaa kufanya msako maalum wa ukaguzi wa vyoo kwa wananchi wote na atakayekutwa hana choo bora apigwe faini ya Tsh 50,000.
Mkuu huyo wa wilaya amelazimika kutoa agizo hilo kufuatia kuwepo kwa taarifa zinazoonyesha kati ya watu watatu katika Manispaa ya Iringa mmoja kati yao anadaiwa kutokuwa na uelewa wa matumizi bora ya choo kwa kuwa hawana uhakika wa kuitumia huduma hiyo ipasavyo.
Akizungumza juzi wakati wa kilele cha siku ya choo Duniani iliyofanyika kiwilaya katika viwanja vya shule ya Msingi Mtwivila maadhimisho yaliyoratibiwa na asasi isiyo ya kiserikali ya ACRA-CCS ,Kasesela alisema anatamani sana kuona wananchi wote wanakuwa na vyoo bora na wanaelimu sahihi ya matumizi ya choo.
Kasesela alisema takwimu zinaonesha kuwa matumizi ya choo bora hupunguza magonjwa ya kuhara kwa asilimia 32 na kunawa mikono kwa sabani hupunguza magonjwa hayo kwa asilimia 50 kuwa sifa za choo bora kuwa ni kile kinachotunza faragha, chenye ubora, kisafi na kinachoongeza heshima kwa mmiliki wake.
" Suala la choo bora ni pamoja na watu kujenga utamaduni wa kunawa mikono na natamani sana kama nyumba zote za ibada zikawa na vyombo maalum vya kunawa mikono pindi waumini wake wanapoingia ibadani ....ila pia shule zikiwa na vyombo vya wanafunzi kunawa mikono kama teknolojia ya chirizi ambayo inatumia maji kidogo zaidi "Akizungumza kwa niaba ya ACRA-CCS, Afisa habari ,Joseph Makanza alisema katika kata hgizo mradi wao unalenga kutambua mifumo ya usafi wa mazingira, kuimarisha mnyororo wa utoaji wa huduma za usafi wa mazingira, kusaidia kubadili tabia katika jamii na kuongeza upatikanaji wa huduma za usafi wa mazingira na maji.
Makanza alisema huduma ya maji na usafi wa mazingira inahusisha matumizi ya teknolojia rahisi nay a bei nafuu kuujenga wa vyoo bora vitakavyomaliza tatizo la baadhi ya watu kujisaidia mahali popote pasipo na huduma hiyo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment