Waziri wa Viwanda na biashara Mhesimiwa Charles Mwijage amewapongeza watengenezaji wa vifaa vya kuhifadhia maji kwa kuendelea kuyaunga mkono malengo ya serikali ya kuanzisha viwanda nchini.
Hayo aliyasema katika hafla ya kuitimisha kampeni ya miezi mitatu ya uza SIMTANK na ushinde na kutoa zawadi kwa mawakala wauzaji wa SIMTANK Bi. Fatina Said na Bw. Rama Jurijs ambao walijishia gari kila mmoja iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
“Nawaomba SILAFRICA waendelee kuibua na kufikia masoko mapya na kutengeneza bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja wao ikiwa ni pamoja na matumizi ya viwandani na majumbani” alisema Mh. Mwijage.
Viwanda vingi vitakavyoanzishwa nchini vitahitaji kwa kiasi kikubwa vifungashio vya bidhaa zake hivyo pamoja na SILAFRICA kuzalisha matangi ya kuhifadhia maji kuna fursa kubwa ya kiwanda hiki kutumia plastiki kuzalisha hivyo vifungashio. Pia Mh. Mwijage aliwataka mawakala wa SIMTANK kuhakikisha wakaazi wa vijijini wanafikiwa na huduma hii ya vifaa vya kutunzia maji vilivyobora ukilinganisha na vile vya asili yaani mitungi inayowezavunjika wakati wowote.
Pamoja na hayo waziri aliwaomba SIALFRICA kuanzisha mpango wa elimu ya kukusanya na kuhifadhi maji wakati wa mvua ili kuwaepusha wananchi na usumbufu wa kukosa maji kipindi cha kiangazi.
Mkurugenzi mkuu wa SILAFRICA TANZANIA LTD, Bw. Alpesh Patel alimuhakikishia waziri kuwa wako tayari kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa maji na kusema kuwa kampeni ya mwaka huu imekuwa na vipengele saba vilivyoshindaniwa hii yote ni kuonyesha jinsi kampuni inavyowajali mawakala wake na wateje wake kwa ujumla.
Leo SILAFRICA, tunafurahi kuzawadia magari mawili kwa mawakala wetu walifanya mauzo vizuri katika mwaka huu. Zawadi hizi ni ishara tosha kuwa bidhaa zetu zinaamika kwa watanzania na pia tumetoa zawadi kwa mawakale wengine waliofanya vizui katika mauzo yao” alisema Bw. Alpesh.
Ningependa kuwapongeza washindi wa kwanza mwaka huu Bi. Fatina Said na Bw. Jurijs kwa kupata zawadi katika kampeni ya uza SIMUTANK na ushinde ya huu wa 2016. Pia pongezi hizi ziende kwa washinde wengine wote katika siku ya leo na niwatie moyo kuwa tayari kupambana kwaajili ya kampeni ya mwaka kesho.
Baadaya kupewa zawadi hiyo Bi. Fatina Said aliishukuru SILAFRICA kwa kutambua mchango wa mawakala wao na kutoa motisha ili kuendelza jitihada zao. Hafla hii imeenda sambamba na udhati wao katika kuwasaidia mamilioni ya watanzania katika lindi zima la ukosefu wa maji.
“Kwangu mimi ushindi si muhimu sana bali kuendelea kuwauzi wateja wangu bidhaa ninazoamini ni borana zinazokidhi mahitaji yao. Hivyo SIMTANK ni bidhaa ambayo wateja wetu huamini” alisema Bi. Fatina.
Naye Bw. Said” alisema wateja wake wengi huuhitaji huduma ya SIMTANK na hii humfanya ajisikie vizuri na ndiyo sababu toka aanze biashara hajasita kuuza matanki haya. Ni bidhaa bora na yenye kupendwa hata katika nchi jirani.
Chapa ya SIMTANK ilizinduliwa nchini Tanzania miaka 20 iliyopita kwa lengo la kuzalisha bidhaa safi, imara, na salama za kutunzia maji. Kwa sasa imekuwa ikiaminika katika soko kwa sababu ya ubora wa teknolojia na malighafi zinazotumika katika utengenezaji wake.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wa pili kulia akimkabidhi funguo za gari mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi la FMJ, Fatima Said baada ya kuibuka mshindi wa mauzo ya bidhaa za tangi la maji aina ya Simtank, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Simtank, Alpesh Patel na kulia ni mshindi mwengine wa shindano hilo Ramadhani Sakalani
Mh. Mwijage akisalimiana na mshindi wa gari katika kampeni ya uza SIMTANK na ushinde Bw. Ramadhani Sakalani. Wakitazama kushoto ni Bw. Alpesh Patel na Bi. Fatina Said.
Bw. Ramadhani Sakalani akionyesha ufunguo wa gari aliloshinda baada ya kukabidhiwa na Mh. waziri.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage wa nne kulia akifafanua jambo mara baada ya kukabidhi funguo za gari kwa mmiliki wa duka la vifaa vya ujenzi la FMJ, Fatima Said baada ya kuibuka mshindi wa mauzo ya bidhaa za tangi la maji aina ya Simtank.
Picha ya pamoja
Bi Fatina Said akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aliyopata kwa kuvuka malengo ya mauzo ya SIMTANK kupitia kampeni ya uzxa na ushinde.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha SILAFRICA baada ya kuwasili katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa Uza SIMTANK na ushinde.
No comments:
Post a Comment