Thursday, December 22, 2016

MAAMUZI YA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA BAADA YA POLISI KUMKATA KHALFAN LIUNDI

whatsapp-image-2016-12-22-at-11-22-22
Mapema asubuhi ya leo Desemba 22, 2016 Wanahabari Mkoani Arusha wamepitisha Azimio maalum kwa wanahabari wote wa Mkoa huo kutoripoti habari ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi ambaye yupo Mkoani  humo kwa shughuli za kiserikali. Azimio hilo ni mpaka pale mwanahabari mwenzao Khalfan Liundi ambaye ni mwandishi wa kituo cha ITV Mkoani  Arusha aliyekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kile kilichoeleza kurusha habari za uchochezi.
Katika taarifa yao waliitoa mapema leo kupitia mtandao wa WhatsApp wa Wanahabari Tanzania (WANAHABARI TZ) ilieleza:  “Azimio lililopitishwa na waandishi wote wa Arusha ni kwamba Mwandishi yoyote atakayeenda kufanya ‘coverage’ ya Lukuvi Leo atatengwa. Tunaombwa kuungana USA River kituo cha Polisi kushinikiza mwenzetu Halfan atolewe mahabusu.” Ilieleza taarifa hiyo.
Hata hivyo taarifa za awali zilieleza kuwa mwandishi huyo alitakiwa kupelekwa Mahakamani ambapo kupitia wanahabari wa mkoa huo, Wakili aliyewekwa na THRDc alipoenda kuongea na Khalfan Liundi, OCSID akakataza Wakili kuongea na Mteja wake lakini baadae OCSID alikanusha juu ya kosa la Uchochezi na kuelezwa kuwa yupo ndani kwa oda ya Mkuu wa wilaya.
Mpaka sasa Wanahabari kwa umoja wao bado wapo katika kituo hicho cha Polisi kusubiria hatima ya mwanahabari huyo, Mo blog itaendelea kukupatia kila kinachoendelea huko.
Unaweza kusoma zaidi tukio hili: http://bit.ly/2i4cPaL
Na Mwandishi Wetu Arusha
itv
Mwandishi Khalifan Liundi

No comments:

Post a Comment