Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo wakati wa uhai wake
Rc Mongela akimpa pole Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimpa pole MD Kayombo.
Na Mathias Canal, Mwanza
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela ameongoza mamia ya wananchi
waliojitokeza kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa
ajili ya kusindikiza safari ya mwisho ya kurejea mavumbini kwa utimilifu
wa vitabu vitakatifu vya Dini Mzee Anton Raphael Kayombo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela akiteta jambo na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Ndg Eliud Mwaiteleke kulia ni Mbunge
wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
Rc Makonda akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Rc
Mongela alisema kuwa kifo cha Mzee Kayombo kimeacha alama kubwa Duniani
kwa ufanisi mkubwa alioufanya akiwa hai ambapo pia ni alama kubwa ya
taswira ya fikra huru zitakazoishi kwa Yale aliowaasa wananchi katika
maelekezo mbalimbali ikiwemo ushauri katika serikali.
Mongela
aliyeambatana na mkewe katika mazishi hayo amewapongeza wananchi wote
kwa kujitokeza mwenye mazishi hayo sambamba na kuwasihi kuendelea kutoa
mshikamano kwa serikali katika majukumu mbalimbali ikiwemo kusimamia na
kudumisha umoja waliouonyesha katika mazishi ya Mzee Kayombo.
Dc Happi akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamini Sitta akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kijijini Misasi
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda alisema kuwa
Mkoa wa Mwanza umepoteza mtu muhimu ambaye atakumbukwa kwa kazi njema
alizozifanya wakati wa uhai wake ikiwemo kuwa mlezi bora wa familia yake
na hatimaye kupatikana kwa kiongozi bora na mwenye weledi katika
utendaji kazi.
Akizungumza
kwa niaba ya kundi la mtandaoni (Watsup) la The Impossible is
Impossible Bwana Steve Nyerere ametoa pole kwa Mkurugenzi wa Ubungo
Ndugu John Lipesi Kayombo kwa kuondokewa na Mzee wake ambaye ni Mlezi
wake tangu akiwa mdogo sambamba na kuwasihi wananchi kuendeleza
mshikamano na kupendana.
Rc Makonda akitoa salamu za pole kwa niaba ya Viongozi wengine alioambatana nao kutoka Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa salamu za shukrani akiwa na Mkewe
Naye
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
alisema kuwa Mzee wake Hugo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali
aliyoyafanya wakati wa uhai wake pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja
na kupanda miti katika shule zote alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati
huo, pia atakumbukwa kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Misasi.
Ameeleza
kuwa Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo alikuwa anasumbuliwa na
ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na
kupelekwa katika hospital ya Misasi, Baadae hospitaliti ya Sekou Ture na
mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata
hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe
4/2/2017 majira ya saa mbili usiku.
Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya Kiserikali ya METDO Tanzania (Mining and Environmental Transformation for Development Organization) Bw Ashraf Omaryakisaini kitabu cga wageni
Muwakilishi
wa kundi la mtandaoni (Watsup) la The Impossible is Impossible Bwana
Steve Nyerere akitoa salamu za pole kwa niaba ya wajumbe wa kundi hilo
Rc Mongela akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Akizungumza
kwa niaba ya wakurugenzi wote nchini Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Kiyomondi Kibamba alisema kuwa msiba huo umekuwa pigo kwa familia ya
Kayombo na ukoo mzima lakini pia ni pigo kwa wananchi wote wa Kijiji cha
Misasi na Mkoa wa Mwanza kwa ujumla kwa kumpoteza mlezi na mshauri
mzuri.
MD
Kayombo amewashukuru madaktari wa hospitali zote waliojaribu kuokoa
uhai wa Mzee Raphael Kayombo hata hivyo ameeleza kuwa idadi kubwa ya
watu waliohudhuria Kwenye mazishi imeonyesha kwamba Marehemu Mzee
Kayombo alikuwa na mahusiano na kuishi vizuri na majiraji zake.
Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo ameacha watoto10, Wajukuu 60 na Vitukuu 30 huku kukiwa na idadi kubwa ya vilembwe.
No comments:
Post a Comment