Wema
Sepetu akishuka katika gari ya Polisi huku pembeni Mbunge wa Singida
Mashariki Tundu Lisu akipunga mkono akitokea katika gari hiyo kwa mbele.
Na Karama Kenyunko,Globu ya Jamii.
Mahakama
ya hakimu Mkazi Kisutu imewaachia kwa dhamana msanii maarufu nchini
Wema Sepetu na wenzake wawili baada ya kutimiza masharti ya kuwa na
wadhamini wawili ambaye kila mmoja atasaini bondi ya Sh milioni tano.
Baada
ya kutimiza masharti hayo, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo Thomas
Simba aliwataka washitakiwa kuhakikisha hawaruki dhamana waliyotakiwa na
kuhakikisha wanafika mahakamani hapo kila wanapohitajika.
Hata hivyo, aliwataka mawakili wa serikali kukamilisha upelelezi haraka ili kesi hiyo ifike mwisho. Mbali na wema washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa ambaye ni mfanyakazi wa ndani na Matrida selemani Abas ambaye ni Mkulima.
Wote
watatu wanashtakiwa na kosa la kukutwa na kiasi kidogo cha madawa ya
kulevya chini ya kifungu cha sheria namba 17 (1)(b) cha sheria
inayodhibiti matumizi ya dawa za kulevya.
Kwa
mujibu wa kifungu hicho, iwapo Wema na wenzake watapatikana na hatia
basi watatakiwa kulipa faini isiyozidi sh.laki tano au kwenda jela.
Akisoma
hati ya mashtaka, Wakili wa serikali Nassoro Katuga aliyekuwa
akisaidiana na Wakili Pamela Shinyambala walidai kuwa Wema na wenzake
watatu walitenda kosa hilo tarehe 4 February mwaka huu, huko nyumbani
kwao Kunduchi Ununio.
Ilidaiwa
kuwa, siku hiyo walikutwa wakiwa na msokoto mmoja pamoja na vipisi
viwili vya banfi vyenye gramu 1.80. Hata hivyo washtakiwa wote wamekana
mashtaka.
Akielezea
hali ya upelelezi wakili Katuga alidai "mheshimiwa Hakimu, upelelezi wa
shauri hili bado haujakamilika tunasubiri taarifa kutoka kwa Mkemia
Mkuu ambayo tunategemea kuipata hivi karibuni".
Hakimu
Simba aliwapa washtakiwa masharti ya dhamana ambapo mahakama ilimtaka
kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakao weka dhamana na milioni
tano. Mshtakiwa Wema na Wenzake walitimiza masharti ya dhamana na kesi
hiyo itatajwa tena mahakamani hapo February 22 mwaka huu.
Nje
ya Mahakama Umati wa watu na wasanii mbali mbali walijaa nje kumlaki
Wema akitoka mahakamani baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Wema Sepetu akitolewa kutoka mahabusu ya Hakimu Mkazi Kisutu
Wema Sepetu akishuka katika ngazi za Mahakama ya Hakimu mkazi kisutu mara baada ya kuamuriwa apte dhamana ya mahakama.
Weme sepetu akipanda kwenda kusaini hati ya Dhamana kwa hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu
Wema akishuka katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu
Wema Sepetu akiwa nje na kwa dhama akiwa ameongozana na wakili
Wema akirudi mahabusu ya hakimu mkazi kisutu akiwa chini ya ulinzi
Meneja wa Wema, Martin Kadinda akitoka mahakamani
Baadhi ya wasanii waliofika mahakamani hapo
Mama wema akiwa naingia mahakamani
No comments:
Post a Comment