Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
Abiria
wa walioshushwa katika basi la Shukurani Coach linalofanya safari zake
Dar kuelekea mikoa ya Kusini wamesema ukaguzi unaofanyika katika kituo
cha mabasi ubungo ni mzuri kwani safari yao isingekuwa nzuri kama
wangeweza kupita bila kukaguliwa.
Akizungumza
na Michuzi Blog, Shinza Lymo amesema kuwa utaratibu wa ukaguzi kabla ya
basi kondoka uendelee kwa wamiliki watakuwa hawapeleki basi katika
kituo hicho na kuwa wameweepusha abiria na ajali zinazotokana na uzembe.
Nae
Halima Bakari amesema kuwa katika siku ambayo hatasahau ni kuzuiwa kwa
basi hilo ambapo leo kitu ambacho kingetokea ni makosa ya watu kushindwa
kufanya matengenezo ya mabasi wakati yanaingia katika kituo hicho .
Amesema
jeshi la polisi wamekuwa makini katika kuhakikisha wanaokoa roho za
watu ambao wanasafiri na vyombo vya moto hasa mabasi ya mikoani ambayo
basi moja linabeba roho 100.
Kwa
upande wa dereva Simwanzi Minja amesema kuwa jeshi la polisi
limenyoosha wamiliki wa mabasi ambao hawataki kupeleka mabasi yao
Gereji na kituo cha ukaguzi wa mabasi cha ubungo kinazua safari.
Amesema
kuwa kutokana na ukaguzi huo ajali zimepungua zinazotokana na mabasi
mabovu kubaki matatizo ya kibinadamu ambayo nayo yamedhibitiwa ipasavyo.
Chami
amesema kuna siku alimwambia mmiliki wa basi kuwa basi lake
linamatatizo alikata na kuamuka kuita polisi kufanya ukaguzi ili
walizuie kufanya safari kabla hajafanyiwa ukaguzi akiwa na abiria.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo akipata maelezo kwa Mkuu
wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo, Ibrahim
Samwix a juu ya ukaguzi wanaofanya kabla ya mabasi hayo kuondoka
kuelekea mikoani alipofika kituo hicho kwa shughuli za kawaida.Picha
zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo akimueleza Mkuu wa
Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo, Ibrahim
Samwix juu ya utaratibu wanaoufanya katika ukaguzi wa magari na
kuwapongeza kwa hatua wanazozichukua kwa basi itakayoonekana na tatizo
leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Geita ,Mponjoli Mwabulambo akiangalia ukaguzi
unaofanywa katika kituo cha mabasi ubungo kabla ya mabasi hayo
hayajaanza safari leo jijini Dar es Salaam na Basi hilo ni Shukrani
Coach ambalo limezuiliwa kufanya safari zake leo baada ya kubaini
usukani wake hauko leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo, Ibrahim
Samwix akikagua injini ya basi kabla halijaanza safari zake leo ubungo
jijini Dar es Salaam.
.Abiria
akilalamikia kurudishiwa nauli katika basi alilotaka kusafiri nalo leo
ambalo limerudishwa kituoni kutokana na kuwa na matatizo kwenye injini
yake kabla halijaanza safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo, Ibrahim
Samwix aking’oa namba za usajili katika basi CM Millenium linalofanya
safari za Dar es Salaam kuelekea Mtwara baada ya kubaini basi hilo
linatatizo na baadae baadae limekufa injini yake kabla halijaanza
safari zake leo ubungo jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo, Ibrahim
Samwix (katikati) akitoa maelekezo kwa askari wake leo katika kituo
cha ubungo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment