Mkuu
wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wikiendi hii alipata nafasi ya
kutembelea nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward
Moringe Sokoine huko Monduli juu Wilayani Monduli.
Mh.Gambo
alipata wasaaa wa kuzungumza na wajane wa kiongozi huyo mkubwa wa
Kitaifa aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 1984 eneo la Dumila huko
Mkoani Morogoro, Mkuu
wa mkoa alipata wasaa wakuzungumza na familia hiyo pamoja na wakazi
majirani wanaozunguka familia hiyo na kusema maneno machache ambapo
Alisema
"Kutembelea
maeneo haya ambapo zipo kumbukumbu za mashujaa wetu waliolipigania
Taifa letu kwa uzalendo mkuu, inatusaidia sisi viongozi vijana kuzirudia
hadhiri zetu za uongozi ili tuweze kuwatumikia wananchi wanyonge kwa
Uadilifu na uwajibikaji,ili kuacha alama katika nafasi tulizopewa na
kuwatumikia wananchi kama walivyofanya wazee wetu hawa."
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,Akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine.
Kutoka Kulia ni Diwani wa Monduli juu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Monduli na pia ni Diwani wa Monduli Mjini Mh:Issack
Joseph,akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine .
Mh:
Gambo akiwa ameambatana na Mjane wa Sokoine Pamoja na watumishi
mbalimbali wa Serikali,Wakitoa Heshima kwenye kaburi la Hayati Sokoine.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh: Mrisho Gambo akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Sokoine.Picha na Msumbanews.com
No comments:
Post a Comment