Shirika
la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limeahidi
kuendelea kuzisaidia redio jamii kwa lengo la kuhakikisha sauti za
wanyonge zinapazwa na kusikika ili kukuza demokrasia nchini. Akizungumza
katika Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania
(COMNETA), Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues alisema UNESCO alisema kuwa wakati umefika kwa wadau wa sekta
ya habari kufikiri kwa kina namna ya kuhabarisha umma kwa kuangalia
namna ya uwasilishaji ambapo kwa sasa changamoto kubwa ni kasi ya ukuaji
wa teknolojia ya habari na namna ambapo redio zinaweza kushindana na
vyombo vingine.
Alisema
kwa wanahabari wanapaswa kuwa makini na taarifa wazitoazo kwa jamii
kwani kumekuwa na mazoea ya baadhi yao kuripoti habari bila kufanya
uchuinguzi wa kina huku wakitumia chanzo kimoja cha habari badala ya
kujiuliza maswali mengi ili kupata taarifa sahihi.
Mkuu
wa Idara ya Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Ofisi za Tanzania,
Christophe Legay akizungumza machache wakati wa mkutano mkuu wa wajumbe
wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA)
unaoendelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es
Salaam.
Aliwashauri
wanachama wa COMNETA, wawe na umoja, mshikamano na kupendana ili
kuepuka migogoro inayoweza kuyumbisha ustawi wa mtandao huo. “Ninawaomba
sana, COMNETA, muwe mfano wa kuigwa kwa kuepuka migongano ya wenyewe
kwa wenyewe ikiwamo kugombea madaraka ili kuwa umoja wa mfano kwa katika
tasnia ya vyombo vya habari hapa nchini’.
‘Vipindi
mbalimbali vya kuhamasisha maendeleo vinavyorushwa na redio hii
vimesaidia sana kuhamasisha wananchi na sasa mwamko wa maendeleo umekuwa
mkubwa hapo Micheweni” alisema Zulmira Rodrigues
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera akizungumza na
wadau mbalimbali wa vyombo vya habari jamii waliokutana kwenye mkutano
mkuu ili kujadili changamoto na kufanya uchaguzi wa viongozi wapya
uliodhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu,
Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Mwenyekiti
wa Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA, Prosper Kwigize
alisema kuwa ipo changamoto kwa baadhi ya maafisa habari mikoani na
wilayani kuleta urasimu mkubwa katika utoaji wa taarifa zinazohitajika
kwa waandishi wa habari hivyo kukwamisha upatikanaji wa habri kwa umma.
Pia kuna changamoto mbalimbali kwenye chama hicho hivyo ni vyema
kuzitafutia suluhiso la msingi ili mtandao huwe imara.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya COMNETA, Mohamed Tibanyendera alisema kuwa kwa
siku za nyuma redio ilikuwa ni chombo cha kuaminika katika utoaji wa
habari hivyo kujijengea umaarufu na kuaminika zaidi tofauti na ilivyo
sasa ambapo kuna upotoshaji mkubwa. Pia aliweza kuyatolea majibu maswali
yaliyoulizwa na wajumbe wa bodi ya COMNETA ili kuimarisha uwajibikaji
katika Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania-COMNETA.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA),
Prosper Kwigize akizungumza na viongozi wa vyombo vya habari jamii
wakati wa mkutano mkuu wa COMNETA unaondelea katika ukumbi wa Chuo Kikuu
Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa Bodi ya Udhamini ya COMNETA, Balozi Christopher Liundi akizungumza
jambo wakati wa mkutano mkuu Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania
(COMNETA) unaofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini
Dar es Salaam chini ya udhamini wa UNESCO.
Katibu
wa Bodi ya Mtandao wa Vyombo vya Habari Jamii Tanzania (COMNETA), Marco
Mipawa akisoma marejesho kwenye mkutano mkuu unaondelea OUT jijini Dar
es Salaam. Pichani
juu na chini ni Baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya COMNETA ambao pia ni
Mameneja na wawakilishi wa vituo vya redio jamii nchini wakishiriki
kutoa maoni kwenye mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea katika ukumbi wa
Chuo Kikuu Huria (OUT) jijini Dar es Salaam.
Kutoka
kushoto ni Afisa Programu wa Mawasiliano na Habari wa UNESCO, Nancy
Kaizilege na Mkufunzi wa Redio Jamii UNESCO, Rose Haji Mwalimu
wakirekodi mambo muhimu katika mkutano mkuu wa COMNETA unaoendelea
jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment