Wednesday, March 22, 2017

KAIRUKI ATEMBELEA SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA NA WALENGWA WA TASAF MKOANI MBEYA.


 Mhe. Kairuki akimsikiliza mmoja wa watumishi wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya nyanda za juu kusini jijini Mbeya alipowapa fursa watumishi hao kutoa maelezo ya vikwazo wanavyopambana navyo .
 Katibu wa Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma , Erick Mbembati (aliyevaa suti nyeusi) akimwonyesha Mhe. Angellah Kairuki kiwanja kinachotarajiwa kujengwa Ofisi za sekretarieti hiyo jijini Mbeya.
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, mhe. Angellah Kairuki akifungua bomba la maji lililojengwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii- TASAF – katika kijiji cha Majengo katika wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, wa kwanza kushoto ni mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga.
 Waziri Kairuki akimwangalia Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga anayekunywa maji kutoka kisima kilichochimbwa na TASAF katika eneo la Majengo ,Wilayani Mbarali ,mkoani Mbeya.
 Waziri  Angellah Kairuki akikagua kwa dhati moja ya kitambusho cha mlengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini unaotekelezwa na TASAF katika kijiji cha Majengo ,wilaya Mbarali mkoani Mbeya wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani hu. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF , Ladislaus Mwamanga.
 Hapa ni furaha kubwa,Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya Utumishi wa umma na utawala bora, Angellah Kairuki akiwa ameketi katika nyumba iliyojengwa na mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Majengo, Gervas  Ngei (mwenye shati ya drafti) kushoto kwa Waziri ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga aliyevaa miwani.
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walengwa wa TASAF Bw. Gervas nje ya nyumba aliyoijenga kwa kutumia fedha za ruzuku zinazotolewa na Mfuko huo kwa takribani kaya milioni MOJA NA LAKI MOJA nchini kote. Mwenye suti nyeusi ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF, Ladislaus Mwamanga.
 Waziri Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa TASAF na halmashauri ya wilaya ya Mbarali nje ya nyumba iliyojengwa na mmoja wa walengwa wa Mfuko  huo  katika kijiji cha Majengo , Gervas Ngei  kwa kutumia fedha alizozipata baada ya kulima mpunga kwa ruzuku hiyo.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora, Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma Kanda ya Nyanda za juu kusini jijini Mbeya.

BALOZI MERO AWASILISHA HATI ZA UTAMBULISHO

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Modest J. Mero akitoa maelezo mafupi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres kabla ya kuwasilisha rasmi Hati za Utambulisho.
Balozi. Modest J. Mero akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres.
Balozi. Modest J. Mero na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres wakipeana mikono baada ya zoezi la kuwasilisha Hati za Utambulisho kukamilika
Balozi. Modest J. Mero na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. António Guterres wakisalimiana na maafisa wa Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa waliokuwepo kushuhudia tukio la kukabidhi Hati za Utambulisho (pichani wakisalimiana na Bw. Songelael Shilla, Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York).
Akizungumza baada ya makabidhiano ya Hati za Utambulisho, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Guterres alisema Umoja wa Mataifa unaishukuru Tanzania kwa jinsi inavyojitolea kwa hali na mali katika jitihada za kumaliza migogoro ya kisiasa katika Ukanda wa Maziwa Makuu. 

Alitaja hatua zinazochukuliwa na Tanzania kurejesha amani DRC, Burundi na Sudan Kusini kuwa ni mfano wa kuigwa na kwamba anayo imani kwamba jitihada hizo hazitakoma mpaka nchi za SADC na EAC zote ziwe na utulivu wa kisiasa.Naye Balozi Mero akitoa neno la shukurani, alimuahidi Bw. Guterres ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa katika kufanikisha malengo ya maendeleo na ulinzi wa amani. 

Aidha, alimwonyesha matarajio iliyonayo Tanzania kwake kwa kuzingatia ushirikiano mzuri aliounesha wakati alipokuwa akishughulikia masuala ya wakimbizi duniani, ambapo kwa pamoja na serikali ya Tanzania waliweza kutekeleza mengi kwa mafanikio makubwa

No comments:

Post a Comment