Watu 9 hawajulikani waliko huku 44 waliokolewa baada ya mashua yao ya uvuvi kuzama nje ya pwani ya kisiwa cha Zanzibar.
Makarani Mohamed, ambaye ni kaimu mkurugenzi ya kitengo cha ujajususi aliambi BBC kuwa shughuli ya kutafuta na kuwaokoa watu bado inaendelea.
"Tunafahamu, kuwa ajali hiyo ilisababishwa na upepo na mawimbi makali yaliyosababisha mashua hiyo kuzama. Alisema.
Manusura mmoja waliwaambia waokoaji kuwa takriban watu 53 waliondoka kuwenda kuvua samaki jana jioni wakati bahari ilikuwa tulivu.
- Watu kadha wafa kwenye ajali ya mashua Tanzania
- Meli kubwa ya Korea Kusini yatoweka baharini
- Gari la Uber linalojiendesha lahusika katika ajali Marekani
Lakini hali ya hewa ilibadilika na kusababisha mawimbi makali ya bahari.
Alisema kuwa hajawaona wenzake tangu ajali hiyo itokee.
Uvuvi ni shughuli kubwa ya kiuchumi katika kisiwa cha Zanzibar lakina mashua nyingi huwa zimechakaa hali ambayo husababisha ajali nyingi.
No comments:
Post a Comment