Mfanyakazi mmoja alirudi katika kiwanda alichokuwa akikifanyia kazi bbada ya kufutwa na na kuwaua kwa kuwapiga risasi kichwani waliokuwa wafanyakazi wenzake kabla ya kujiua.
John Rubet Neumann 45 alikuwa amejihami kwa bunduki na kisu wakati aliingia katika biashara moja karibu na Orlando huko Florida siku ya Jumatatu asubuni
Mwanajeshi huyo wa zamani wa Marekani alifutwa kazi mwezi Aprili, kwa mujibu wa polisi.
Wengi wa wale waliouwawa walipigwa risasi kichwani.
Alikuwa akiwachagua wale aliowapiga risasi, polisi walisema.
Waliouwawa ni pamoja na Robert Snyder, 69, Brenda Montanez-Crespo, 44, Kevin Clark, 53, Jeffrey Roberts, 57, na mtu mwingine ambaye hakutambuliwa.
Mtu huyo alimuambia mfanyakazi moja ambaye hakuwa anamjua aondoke eneo hilo.
Neumann aliyekuwa anaishi peke yake eneo hilo, alijiua wakati polisi walikuwa wanakaribia kuingia katika majengo hayo.
Mamlaka zinasema kuwa hakuwa na leseni ya kumiliki bunduki.
Aliondoka katika jeshi la Marekani mwaka 1999.
No comments:
Post a Comment