tarehe 03.06.2017
majira ya saa 06:00hrs asubuhi katika mtaa wa kitangiri kata ya kitangiri
wilaya ya ilemela jiji na mkoa wa mwanza, kulwa mabula miaka 37, mkazi wa
mtaa wa kitangiri amekutwa akiwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia kamba ya
manila aliyokuwa ameifunga kwenye mti uliokuwa kando ya barabara ya kitangiri,
kitendo ambacho ni kosa kisheria.
inasemekana marehemu
alikuwa na mgogoro wa kimapenzi na mtu aliyekuwa na mahusiano nae, kutokana na
mgogoro huo kudumu kwa muda mrefu ndipo tarehe tajwa hapo juu aliamua kuchukua
maamuzi ya kujitoa uhai.
polisi wapo katika
uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya
rufaa ya bugando kwa ajili ya uchunguzi, pindi uchunguzi ukikamilika
utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa ajili ya mazishi.
kaimu kamanda wa
polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi wa polisi zarau mpangule anatoa wito
kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka kuacha tabia ya kujichukulia
sheria mkononi kwani ni kosa kisheria, bali pindi wanapokuwa kwenye migogoro
aidha ya ndoa au mahusiano au ya aina yoyote ilie wawaeleze wazee wenye busara
na hekima, au mwenyekiti wa mtaa au vyombo vya dola ili kuweza kuepusha vifo
vya aina kama hii ambavyo vinaweza kuzuilika.
katika tukio la pili;
mnamo tarehe
03.06.2017 majira ya saa 10:30hrs asubuhi katika kijiji cha mwanangwa kata ya
mabuki wilaya ya misungwi mkoa wa mwanza, mtu mmoja mwanamume ambaye bado
hajafahamika jina wala makazi anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi
30, aliuawa na kundi la watu waliojichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mawe na
fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kisha baadae kumchoma moto kwa kosa la
wizi wa kuku wawili, kitendo ambacho ni kosa la jinai.
inadaiwa kuwa
marehemu alikamatwa na wananchi akiwa na kuku wawili ambao amewaiba katika moja
ya nyumba kijijini hapo, inasemekana baada ya wananchi wa kijijini hapo
kumkamata walianza kumhoji huku wakimpiga kwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali
za mwili wake kisha baadae kumchoma moto.
watu/ wasiri walitoa
taarifa polisi kuhusiana na mauaji hayo ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa
haraka hadi eneo la tukio, na kufanikiwa kuwakamata watu watano wanaodaiwa
kuhusika kwa namna moja au nyingine katika kufanikisha mauaji hayo. aidha
polisi wapo katika upelelezi na mahojiano na watuhumiwa pindi uchunguzi
ukikamilika watafikishwa mahakamani, mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali
ya wilaya ya misungwi kwa ajili ya uchunguzi na utambuzi.
kaimu kamanda wa
polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi wa polisi zarau mpangule anatoa wito
kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza akiwataka kuacha tabia ya kujichukulia
sheria mkononi pindi wanapowakamata wahalifu kwani ni kosa la jinai, bali watoe
taarifa polisi au wamfikishe mtuhumiwa kwenye kituo cha polisi ili hatua
stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake.
katika tukio la tatu;
kwamba tarehe
03.04.2017 majira ya saa 12:00hrs katika mtaa wa sabasaba kata ya kiseke wilaya
ya ilemela jiji na mkoa wa mwanza, askari wakiwa kwenye doria na misako
walifanikiwa kuwakamata watu watatu wakiwa na madawa ya kulevya, kati yao
wawili ambao ni 1.ally salehe miaka 47, mkazi wa nyasaka na 2.wiliam magoma,
miaka 31, mkazi wa nyasaka, walikamatwa wakiwa na madawa ya kulevya aina ya
bhangi kiasi cha misokoto 52, huku wa tatu aliyefahamika kwa jina la
paschal lusozi miaka 47, mkazi wa nyasaka alikamatwa akiwa na madawa ya
kulevya yadhaniwayo kuwa ni ya heroine kiasi cha pinchi 10, kitendo
ambacho ni kosa kisheria.
awali askari
walipokea taarifa kutoka kwa wasiri kwamba katika mtaa tajwa hapo juu wapo
baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya. kutokana
na taarifa hizo askari walianza kufanya upelelezi na misako katika maeneo hayo
ndipo tarehe tajwa hapo juu watuhumiwa watatu waliweza kutiwa nguvuni
huku wakiwa na aina hizo za madawa ya kulevya.
polisi wapo katika
upelelezi na mahojiano na watuhumiwa wote watatu, pindi uchunguzi ukikamilika
watafikishwa mahakamani, aidha upelelezi na msako wa kuwatafuta watu wengine
wanaojihusisha na biashara haramu za madawa ya kulevya bado unaendelea.
kaimu kamanda wa
polisi mkoa wa mwanza kamishina msaidizi wa polisi zarau mpangule anatoa rai
kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza hususani vijana akiwataka kuacha tabia ya
kujihusisha aidha na uuzaji,utumiaji au usafirishaji wa madawa ya kulevya kwani
ni kosa la jinai, na endapo mtu atabainika hatua stahiki za kisheria
zitachukuliwa dhidi yake. aidha pia anawaomba wananchi wa mkoa wa mwanza
kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa mapema za
imetolewa na;
acp: zarau mpangule
kaimu kamanda wa polisi
(m) mwanza
No comments:
Post a Comment