Saturday, July 15, 2017

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTOAJI WA VYETI VYA WAHITIMU WA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KATIKA PROGRAMU ZA AFYA, MIFUGO NA UALIMU KWA MWAKA WA MASOMO 2015/2016


 
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
  



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge, Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi nchini. 


NACTE ina wajibu wa kutunuku vyeti kwa wahitimu wenye sifa stahiki kwa mafunzo ya programu za Afya, Mifugo na Ualimu yanayozingatia umahiri.


Baraza linapenda kutoa taarifa kwa umma kuwa vyeti vya wahitimu wa mafunzo ya programu za Afya, Mifugo na Ualimu wenye sifa stahiki kwa mwaka wa masomo 2015/16 viko katika hatua za mwisho za uchapaji na vitatolewa muda wowote ndani ya mwezi huu wa Julai 2017.
  
IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE: 14/07/2017

No comments:

Post a Comment