Joseph Ngilisho,Arumeru
HALMASHAURI ya Meru inatarajia kukusanya zaidi ya
shilingi bilion 29, kutoka vyanzo vya mapato ya ndani na nje, kwa ajili ya kuanzisha
miradi ya maendeleo na huduma nyingine za Halmashauri hiyo.
Hayo yamesemwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru,Trasias
Kagenzi wakati alipokuwa akiongelea jinsi walivyojipanga na wadau wa maendeleo
kwa kushirikiana na wananchi kuhakikisha, wanapunguza hali duni za maisha ya
wananchi, kwa kuanzisha miradi ya msingi, kama vile ujenzi wa Barabara
,miundo ya maji ,huduma bora za Afya .
Kagenzi alifafanua kuwa fedha kutoka mapato ya ndani ni shilingi milioni
466,140,000, Uchangiaji wa Huduma za Afya ,shilingi milioni 105,000,000
,Mishahara bilion 20,538,207,000, Ruzuku ya matumizi ya Kawaida, bilion
2,821,901,000,Ruzuku ya miradi ya Maendeleo,sh. milioni 3,603,339,000 na
Michango ya Jamii, Million 366,647,000
Alisema kuwa fedha hizo zitachangia kwa kiasi kikubwa
huduma ya maji ,elimu ,afya na miradi mingine ya msingi
itakayoibuliwa na wananchi katika ngazi ya kata na vijiji .
Aidha alifafanua kuhusu uchangiaji wa wananchi katika miradi ya
maendeleo, kuwa bado ni mdogo sababu baadhi ya wananchi wanashindwa
kuchangia, kutokana na hali duni ya maisha katika maeneo wanayoishi .
Halmashauri ya Meru ni miongoni mwa Halmashauri saba za Mkoa wa Arusha na ni ya
pekee iliyopata hati safi na zingine zikiapata hati za mashaka na Manispaa ya
Arusha kupata hati chafu.
No comments:
Post a Comment