Sunday, May 20, 2012

Huenda Ushoga ukahalalishwa Mali



Rais Joyce Banda wa Malawi ametangaza kuwa anataka kubatilisha sheria iinayopinga vitendo vya ushoga  vinavyokwenda kinyume na desturi za Kiafrika ambapo mashoga hawakubaliki katika jamii na hukabiliwa na mkono wa sheria iwapo watapatikana.

 Banda ambaye alichukua uongozi mwezi wa Aprili baada ya mtangulizi wake Bingwa wa Mutharika kuaga dunia, alitangaza haya katika hotuba yake ya kwanza nchini Malawi.

 Hatamu ya Rais Joyce Banda inamalizika mwaka wa 2014. Malawi ilishutumiwa kimataifa baada ya wanaume wawili nchini humo waliokamatwa mwaka 2010 kuhukumiwa kifungo cha miaka 14 baada ya kutangaza kuwa wanataka kuoana.

 Matamshi ya Banda yamepokelewa vyema na watetezi wa haki za binaadamu nchini humo lakini wametahadharishwa kuwa haitakuwa rahisi kwa rais huyo kuungwa mkono na bunge. Afrika Kusini ni nchi pekee ya Kiafrika yenye sheria zenye kulinda haki za mashoga.   

No comments:

Post a Comment