|
MIGA
|
Taasisi
ya Kudhamini Uwekezaji
TAASISI ZA BENKI YA DUNIA
|
Mfano wa Maelezo Mafupi ya Mradi
Muhtasari
wa mapendekezo ya udhamini hutolewa kabla ya vikao vya maamuzi ya Bodi na kabla
ya hatua ya mwisho ya kusaini mkataba, hivyo huweza kubadilishwa. Muhtasari wa
taarifa za mradi huwekwa bayana baada ya maamuzi ya Bodi na kusainiwa kwa
mkataba, na huakisi vigezo vinavyoambatana na mradi wakati wa kusainiwa mkataba.
Muhtasari wa Mapitio ya Athari za Kimazingira na Kijamii hutolewa kwa miradi
ambayo imeainishwa katika Kundi A au B la Tathmini ya Athari za Mazingira.
Jina la Mradi: Kahama
Mining Corp. Ltd.
Utambulisho wa mradi: 3661
Mwaka wa fedha: 2001
Hadhi ya mradi: Haufanyi kazi
Mdhamini: Kampuni ya Barrick Gold Corp. ya Canada
Nchi ya mwekezaji: Canada
Nchi ya uwekezaji: Tanzania
Sekta: Madini
Thamani kuu ya mradi: Dola za Marekani milioni 56.2
Aina ya Mradi: Non-SIP
Utambulisho wa mradi: 3661
Mwaka wa fedha: 2001
Hadhi ya mradi: Haufanyi kazi
Mdhamini: Kampuni ya Barrick Gold Corp. ya Canada
Nchi ya mwekezaji: Canada
Nchi ya uwekezaji: Tanzania
Sekta: Madini
Thamani kuu ya mradi: Dola za Marekani milioni 56.2
Aina ya Mradi: Non-SIP
Mdhaminiwa
mpya wa MIGA atasaidia kutumia rasilimali ambazo hazijaendelezwa za sekta ya
madini nchini Tanzania, hivyo kusaidia nchi kupanua wigo wake wa uchumi. Katika
mwaka wa fedha 2001, Kampuni ya Barrick Gold Corp. ya Canada ilipokea udhamini
wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 56.25 kutoka MIGA kwa ajili ya
uwekezaji kwenye mgodi wa dhahabu, fedha, na shaba nchini Tanzania. Kampuni binafsi za bima zinatoa uhakikisho
wa udhamini wa uwekezaji huu. Bima hii itakinga uwekezaji dhidi ya hatari za zuio la
kuhamisha faida, kutaifishwa kwa mali, madhara ya vita na fujo miongoni mwa
raia. Shirika la Maendeleo ya Bidhaa Nje
la Canada pia ni mdhamini katika mradi huu.
Mradi
unahusisha kuanzishwa na kuendesha mgodi na mitambo yake. Katika uhai wa mgodi,
mradi unatarajiwa kuzalisha kila mwaka wakia 420,000 za dhahabu, wakia 240,000 za
fedha, na kilo milioni 3.8 za shaba. Mbinu bunifu zinatumika kuondoa mabaki ya
uzalishaji, kutumia teknolojia ya kugandisha madini na kujaza mashimo ya mgodi.
Uwekezaji
utachangia katika maendeleo ya miundombinu ya nchi. Jamii zinazonguka mgodi
zitanufaika moja kwa moja kwa kupata maji kutoka kwenye mabomba yanayojengwa na
wafadhili wa mradi, upatikanaji wa umeme kwa kaya za wanavijiji, na maendeleo
ya barabara.
Mradi
utatengeneza takribani ajira 1,500 wakati wa ujenzi na zaidi ya ajira mpya 1,000
za kuendesha mgodi. Chini ya makubaliano na serikali, mradi utatayarisha na
kutekeleza programu ya ajira na mafunzo kwa wafanyakazi wake wa Kitanzania
katika kila awamu na katika ngazi zote za kuendesha mradi. Mradi utalipa
takribani Dola za Marekani milioni 75 kama kodi, mrahaba na ushuru kwa serikali
wakati wa miaka yake 15 ya mwanzo, na kununua bidhaa na huduma zinazozalishwa
nchini zenye thamani ya takribani Dola za Marekani milioni 10.
No comments:
Post a Comment