|
MIGA
|
Taasisi
ya Kudhamini Uwekezaji
TAASISI ZA BENKI YA DUNIA
|
MIGA
ni moja ya Taasisi zilizo chini ya Benki ya Dunia. Dhamira yetu ni kukuza
uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika nchi zinazoendelea ili kusaidia ukuaji uchumi, kupunguza umasikini, na
kuboresha maisha ya watu.
Mkakati wetu
Mkakati
wa kiutendaji wa MIGA hutumia uwezo tuliokuwa nao katika masoko—kuvutia
wawekezaji na wadhamini binafsi katika mazingira magumu ya kiutendaji.
Tunalenga katika kudhamini uwekezaji pale ambapo tunaweza kuleta mabadiliko
makubwa.
- Nchi ambazo zinastahili kupata msaada kutoka Taasisi ya Maendeleo ya Kimataifa (nchi masikini zaidi duniani)
- Maeneo yaliyokumbwa na migogoro
- Mikataba yenye utata katika miundombinu na uchimbaji madini, hasa ile inayohusisha fedha za kugharamia miradi na masuala ya mazingira na kijamii
- Nchi za Kipato cha Kati ambako tunaweza kuleta mabadiliko
Kuna
faida nyingi katika huduma zinazotolewa na MIGA kwenye maeneo yote haya—kuanzia kwenye huduma zetu
mahususi na uwezo wa kurudisha imani ya wafanyabiashara, hadi ushirikiano wetu
unaoendelea na soko la bima la umma na binafsi, katika kuongeza kiwango cha
bima wanachoweza kupata wawekezaji.
Kama
taasisi ya maendeleo iliyo na wadau wengi, MIGA hutoa msaada pale tu ambapo
uwekezaji huleta mabadiliko kimaendeleo na kukidhi viwango
vya juu vya kijamii na kimazingira. MIGA hutumia viwango vya utendaji kijamii na kimazingira vilivyosheheni
vipengele mbalimbali katika miradi yote na hutoa huduma za kitaalamu kwa
wawekezaji ili kuhakikisha viwango hivi vinazingatiwa.
Bidhaa
zetu
Tunatimiza
dhamira yetu kwa kuwapatia wawekezaji wa sekta binafsi na wanaokopesha udhamini wa bima dhidi ya hatari za kisiasa. Udhamini wa MIGA hulinda
uwekezaji dhidi ya hatari ambazo si za kibiashara ma huweza kuwasaidia
wawekezaji kupata vyanzo vya fedha vilivyo na masharti na vigezo nafuu. Uwezo
wetu wa kipekee unatokana na kuwa moja ya taasisi za Benki ya Dunia, na muundo
wetu kama shirila la kimataifa lililo na wana hisa wanaojumuisha nchi nyingi
duniani. Tangu kuanzishwa kwetu mwaka 1988, MIGA imetoa zaidi ya Dola za
Marekani bilioni 28 kama bima dhidi ya hatari za kisiasa kwa miradi kwenye
sekta mbalimbali katika maeneo yote
duniani.
Pia
tunafanya utafiti na kushirikishana ujuzi kama sehemu ya wajibu wetu wa
kusaidia uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika masoko machanga. Hii
inathibitisha nafasi yetu kama kiongozi wa fikra na chanzo cha habari
zinazohusiana na hatari za kisiasa kwa wafanya biashara wa bima.
Timu yetu
Watu
wetu wana uzoefu mpana katka masuala ya bima ya hatari za kisiasa, wakiwa na
taaluma mbalimbali zikiwemo masoko ya kibenki na mitaji, uendelevu wa kijamii
na kimazingira, fedha za kugharamia miradi na mahitaji mahususi ya sekta, na
sheria za kimataifa na usuluhishi wa migogoro. Kutana na Timu yetu ya maafisa waandamizi wa menejimenti.
Wanahisa wetu
Baraza
la Magavana na Bodi ya Wakurugenzi wanaowakilisha
nchi wanachama huongoza programu na
shughuli za MIGA. Baraza la Magavana ndilo lenye mamlaka ya kitaasisi ya MIGA,
ambalo hugatua madaraka yake mengi kwa Bodi ya Wakurugenzi. Mamlaka ya kupiga
kura hutegemea kiasi cha mtaji ambacho kila mkurugenzi huwakilisha. Wakurugenzi
hukutana mara kwa mara katika makau makuu ya Taasisi za Benki ya Dunia, jijini Washington,
DC, ambako hufanya mapitio na maamuzi kuhusu miradi ya uwekezaji na kusimamia
sera za jumla za menejimenti.
No comments:
Post a Comment