Monday, August 25, 2014

Jinsi MIGA inavyofanya kazi


MIGA
Taasisi ya Kudhamini Uwekezaji 
     TAASISI ZA BENKI YA DUNIA


                                                                Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mfano wa Muhtasari wa Mapendekezo ya Udhamini *
Muhtasari wa mapendekezo ya udhamini hutolewa kabla ya vikao vya maamuzi ya Bodi na kabla ya hatua ya mwisho ya kusaini mkataba, hivyo huweza kubadilishwa. Muhtasari wa taarifa za mradi huwekwa bayana baada ya maamuzi ya Bodi na kusainiwa kwa mkataba, na huakisi vigezo vinavyoambatana na mradi wakati wa kusainiwa mkataba. Muhtasari wa Mapitio ya Athari za Kimazingira na Kijamii hutolewa kwa miradi ambayo imeainishwa katika Kundi A au B la Tathmini ya Athari za Mazingira.
Jina la Mradi:                        Silverlands Tanzania Limited
Utambulisho wa mradi:        12353
Mwaka wa fedha:                 2014
Hadhi ya mradi:                    Umependekezwa
Mdhamini:                             Overseas Private Investment Corporation (OPIC)
Nchi ya mwekezaji:               Marekani
Nchi ya uwekezaji:                Tanzania
Sekta:                                                 Biashara ya kilimo
Thamani kuu ya mradi:       Dola za Marekani milioni 34 
Aina ya Mradi:                      Non-SIP
Muhtasari huu unahusu uhakikisho wa udhamini wa MIGA kwa dhamana iliyotolewa na Kampuni ya Overseas Private Investment Corporation’s (OPIC) kwa ajili ya bima kwa Mfuko wa SilverStreet Private Equity Strategies Soparfi Sarl (hapa inafahamika kama Mfuko)), mfuko wa kilimo unaolenga kwenye uwekezaji barani Afrika kusini mwa jangwa la Sahara. MIGA inalenga katika kutoa uhakikisho wa dhamana kwa OPIC kwa ajili ya uwekezaji wa mfuko huo katika Kampuni ya Silverlands Tanzania Limited (hapa inafahamika kama Mradi). OPIC imeomba uhakikisho wa udhamini wa Dola za Marekani milioni 34.0 kwa kipindi cha hadi miaka 10 dhidi ya hatari za zuio la kuhamisha faida, kutaifishwa kwa mali, madhara ya vita na fujo miongoni mwa raia.
Mapendekezo ya msaada huu wa MIGA kwa OPIC unaendana na mamlaka ya MIGA ya kushirikiana na makampuni ya kitaifa ya nchi mwanachama, kama ilivyotamkwa katika Mkataba wa MIGA.
Mradi unahusisha uwekezaji wa Mfuko wa hadi Dola za Marekani milioni 60 katika Kampuni ya Silverlands Tanzania Limited (STL) kwa ajili ya kununua mali za kampuni mbili za kilimo na kuziunganisha na kuziweka katika vitengo viwili: Kitengo cha Kuku cha Makota, mchanganyiko wa biashara ya kuku; na Kitengo cha Mazao na Mifugo cha Selous. Mfuko unawekeza katika utengenezaji wa vyakula vya mifugo, hifadhi ya mazao katika silo, mabanda ya kufugia na kutagia kuku, mashine za kutotolea vifaranga, na vifaa vingine vinavyohusiana ili kutengeneza biashara inayoongoza ya kuku inayojumuisha vipengele mbalimbali nchini Tanzania.
Uwekezaji wa Mfuko huu nchini Tanzania unasukumwa na mienendo ya jamii inayoibuka ambayo inaakisi ongezeko la watu nchini Tanzania, ongezeko la kipato, na uhitaji wa vyakula vya mifugo ili kukidhi mahitaji ya watu wanaoongezeka ya vyakula vya proteni. Kampuni ya STL inalenga katika uwekezaji katika vituo vingi vya uzalishaji wa bidhaa za proteni nchini Tanzania, ikijumuisha miji ya Iringa na Dar es Salaam, na baada ya hapo kuelnga Masoko yanayokua kwa haraka nchini Tanzania na nchi jirani.
Mradi huu uko katika Kundi B chini ya Sera ya MIGA ya Uendelevu wa Kimazingira na Kijamii. Kliki hapa ili uangalie Muhtasari wa Mapitio ya Kimazingira na Kijamii.
Lengo kuu la maendeleo ya mradi ni kusaidia uendelevu wa sekta ya kilimo kwa kupanua ardhi ya Mtanzania inayolimwa kwa kuendeleza uwezo wa umwagiliaji na maboresho ya michakato na ujuzi wa usimamizi; kuongeza uzalishaji wa mifugo kwa kutumia michakato yenye ufanisi na teknolojia; na kujenga miundombinu ya msingi katika kilimo. Ifikapo mwaka wa tano wa uzalishaji, vitengo hivyo viwili vinatarajiwa kuajiri wafanyakazi wa kudumu wazawa 925, na wafanyakazi wengine 120 wa msimu.
Mapendekezo ya msaada wa MIGA kwa ajili ya mradi unalingana na mkakati wa kitaifa wa maendeleo ya Tanzania, ambao unaainisha kilimo kama kipaumbele kwa ajili ya ukuaji uchumi, kupunguza umasikini, na uhakika wa chakula. Mradi pia unalingana na Mkakati wa Kusaidia Nchi wa Benki ya Dunia kwa Tanzania na Mkakati wa Benki ya Dunia kwa Afrika. Chini ya nguzo ya kwanza ya Mkakati wa Kusaidia Nchi (Kukuza Ukuaji Uchumi Unajumuisha Wote na Ulio Endelevu, Unaoongozwa na Sekta Binafsi) Benki husaidia serikali kuboresha kipato katika sekta ya kilimo kwa kuwasaidia wakulima kutumia mbinu za kilimo zilizo na tija zaidi na ujenzi wa miundombinu ya kilimo.
*Tafadhali zingatia: Wakati mradi huu ukipitishwa hivi karibuni na Bodi ya MIGA, taasisi inasubiri hatua ya mwisho ya mkataba kutiwa saini.

No comments:

Post a Comment