MIGA TAARIFA KWA MUHTASARI
Afrika Kusini mwa Sahara
KUDHAMINI
UWEKEZAJI KUHAKIKISHA
FURSA
Bara linalopiga Hatua
Nchi za Bara la Afrika Kusini mwa jangwa la
Sahara zimeendelea kuwa eneo linalo wavutia wawekezaji. Nchi hizi zimeshuhudia kuongezeka kwa kiwango cha
juu na endelevu katika ukuaji wa uchumi katika miaka ya hivi karibuni, wakati
makadirio yakionyesha kupanuka kwa uchumi kwa asilimia 5 kwa mwaka 2012, ikifuatia kupanuka kwingine kwa kiwango cha
asilimia 4.7 mwaka 2011. Wakati
sekta ya madini imekuwa ndio msukumo mkuu wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa
moja katika bara hili, uwekezaji katika sekta ambazo si za uziduzi pia umekuwa ukiongezeka kutokana
na maboresho ya taasisi za udhibiti, utawala
bora na kwa ujumla mazingira mazuri ya kufanya biashara katika kanda hii—pia
kuongezeka kwa tabaka la kati ambalo huvutia wawekezaji wanaotafuta masoko
mapya.
Hisia za Hatari za Kisiasa Hukwamisha Uwekezaji
Licha ya uwezo wake mkubwa, gharama za
chini za nguvu kazi, na maliasili nyingi, wawekezaji wengi bado wanakuwa na
wasiwasi wa kuwekeza katika bara la Afrika. Bara hili ni eneo lililo na nchi 17
ambazo Benki ya Dunia huzianisha kuwa ni nchi “tete na zilizogubikwa na
migogoro”. Kwa baadhi ya wawekezaji, hatari za
kufanya biashara katika nchi zilizo na usalama mdogo kisiasa mara nyingi ni
kubwa zaidi kuliko faida ya kuingia masoko yenye faida kubwa. Na nchi nyingi za
Kusini mwa Jangwa la Sahara bado zinaonekana kuwa zina hatari kubwa, zenye gharama
kubwa ya kufanya biashara. Hatari ambazo zinawapa wasiwasi wawekezaji na
wakopeshaji mara nyingi zinahusiana na imani ndogo katika mfumo wa mahakama
na taasisi za udhibiti, utawala mbovu, rushwa na uhaba wa utawala wa sheria, kutokuwepo
kwa usimamizi wa mikataba,
machafuko ya kisiasa, na kuyumba kwa uchumi mkuu Hii humaanisha kwamba bara
linakabiliwa na uwezekano wa kupoteza mitaji ambayo ni muhimu kwa kukuza
uchumi, na kwa wawekezaj kukosa fursa za kugema kiwango kikubwa cha
bidhaa/madini kutoka kwenye soko changa ambalo bado kwa sehemu kubwa
halijashughulikiwa.
MIGA inaweza Kusaidia
MIGA inaweza
kusaidia nchi za Kusini mwa Sahara kuvutia uwekezaji ambao hujenga ajira na
kuchangia katika ukuaji uchumi na kusaidia wawekezaji kupata faida kutokana na
mchakato huo. Jukumu la MIGA ni kusaidia ukuaji uchumi, kupunguza
umasikini na kuboresha maisha ya watu kwa kukuza uwekezaji wa kigeni wa moja
kwa moja katika nchi zinazoendelea. Tunafanya hivyo kwa kutoa bima dhidi ya
hatari za kisiasa (au wadhaminiwa), dhidi ya aina fulani za hatari ambazo si za
kibiashara katika nchi zinazoendelea Ikiwa moja ya Taasisi mojawapo za Benki ya
Dunia, MIGA iko katika nafasi nzuri zaidi ya kusaidia kutatua migogoro ambayo inaweza kutokea baina ya wawekezaji na
serikali za nchi mwenyeji MICA pia inafanya kazi kwa karibu na Benki ya Dunia
na Shirika la Kimataifa la Fedha kuupa uwezo uwekezaji wa sekta binafsi,
hususani katika miradi mikubwa ya miundombinu ambayo inahitajika kwa haraka
zaidi ili kuweka misingi ya ukuaji uchumi.
MIGA haiweki kikomo cha ukubwa wa miradi
inayosaidia Kwa uwekezaji mkubwa, MIGA inaweza kuhamasisha kiwango cha udhamini unaohitajika
MIGA hutoa huduma za bima kwa uwekezaji wa kigeni wa
moja kwa moja dhidi ya hasara zinazohusiana na:
§ Zuio la kuhamisha na kubadilisha fedha za
kigeni
§
Kutaifishwa kwa mali
§ Vita, fujo za raia, ugaidi na hujuma
§
Kuvunjika kwa mkataba
§ Kutokuheshimu masharti ya fedha ya nchi huru
MIGA TAARIFA KWA MUHTASARI
Afrika Kusini mwa Sahara
KUDHAMINI
UWEKEZAJI KUHAKIKISHA
FURSA
MIGA katika nchi za

No comments:
Post a Comment