Baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani nchini
Uganda wamemuandikia barua Rais Yoweri Museveni wa nchi hiyo wakimtaka ajiuzulu
ndani ya siku 60 la sivyo wamtoe kupitia sheria za bunge.
Wabunge hao wakiongozwa na Ibrahim Ssemuju wa jimbo
la Kyaddondo Mashariki na Odonga Otto wa jimbo la Aruu wamesema Rais Museveni
ametenda makosa ya jinai mengi
zaidi za kiuchumi na hivyo hafai kuendelea kuongoza.
Wabunge hao wawili wamekabidhi barua hiyo kwa ofisi
ya Rais kwa niaba ya wenzao, Ikulu ya Rais imepuuzia mbali barua hiyo na
kuitaja kuwa upuuzi wa wabunge waliokosa kazi ya kufanya,
Sehemu moja ya barua hiyuo inasema "Bw. Rais,
kutokana na umri wako mkubwa na kwa kuzingatia makosa ya jinai uliyowatendea
wananchi wa Uganda, tunakutaka uchukue uamuzi wa kujiuzulu ndani ya miezi
miwili ijayo la sivyo tutatumia sheria za bunge kukung'oa madarakani".
Kambi ya upinzani imeshindwa kukusanya saini zinazotakikana kisheria ili
kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na rais katika bunge la nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment