Tuesday, January 21, 2014

HUYU NDIO MWANAJESHI FEKI ALIYETIWA MBARONI JIJINI TANGA




KOPLO FEKI  akichukuliwa na LUTENI Yahaya Wangwe na mteule daraja la pili Albano Semfuko.



Vikosi vya usalama jijini Tanga, vinamshililia  Edwin John Mponyi mwenye umri wa miaka 31 kufuatia kwenda kwenda kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tanga na kujitambulisha kuwa yeye ni koplo wa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ, Akitaka kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa katika jeshi la kujenga Taifa.

koplo mponji alikwenda katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya tanga, Halina Dengego, mnamo january 16 mwaka huu ambapo kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapo ilikuwa ikifanya usaili wa kupata vijana wa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa.JKT.

Akiwa katika ofisi ya mkuu wa wilaya ,koplo Mponji alijitambulisha kuwa  yeye ni afsa wa JWTZ ambaye
 kwa sasa yupo katika kikosi cha 36 KJ kilichopo mkoani Pwani akiwa ameambata na kijana Emmanuel Joseph  akitaka afanyiwe  mpango ili apata nafasi katika jeshi la kujenga taifa.

Hata hivyo wakati akitoa maelezo hayo ,mshauri wa mgambo wilaya ya Tanga ,sir Meja Albano Semfuko ,alimtilia shaka na kumjulisha mkuu wa mkoa ambaye alitoa amri koplo huyo ashikiliwe kwa mahojiano zaidi.

Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa wilaya anasema baada ya mahojiano  walibaini kuwa Mponji hakuwa askari wa JWTZ,Ndipo walipolazimika kumpeleka nyumbani kwake mtaa wa Magomeni jijini TANGA ambapo  baada ya upekuzi walikuta nguo za jeshi zikiwa na cheo cha koplo.

Wakati Mponji anakamatwa alikuwa na kaptura ya jeshi lakini baada y a kupelekwa kituo cha polisi chumbageni ,walifanya njama ya kuivua na kumpa mahabusu ambaye al;ikuwa anatoka hivyo kutoweka nayo.

Mponji alionyeshwa mbele ya waandishi wa habari ,ambapo alihojiwa na kushindwa kujieleza ipasavyo  kuhusu ni wapi na mahali gani alipopota hizo sare za jeshi ,ingawa alikuwa kuwahi  kumaliza mafunzo  katika jeshi la kujenga taifa kikosi cha 841 KJ Mafinga.

Kufuatia tukio hilo mkuu wa wiliaya ya Tanga ameamuru jeshi  la wananchi Tanzania kufanya uchunguzi juu ya koplo feki mponji ili kubaini mtandao wao

No comments:

Post a Comment