Saturday, May 26, 2012

LORI LENYE MAGUNIA 50 YA BANGI LAKAMATWA ARUSHA







WATU wanne wametiwa mbaroni na jeshi la polisi katika ‘njia ya panya’ mpakani mwa Tanzania na Kenya, mkoani Arusha baada ya kukutwa na magunia 50 ya bangi yenye thamani ya mamilioni ya fedha wakiwa njiani kupelekwa Kenya.

Waliokamatwa ni pamoja na wakulima Babuu Laizer (34) na Lomnyaki Lekibengi (30), dereva wa lori dogo aina ya Toyota DCM lenye namba za usajili T922 AFJ lililokamatwa likiwa na mzigo huo, Edward Mollel na utingo wake, John Joshua (36).

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Arusha, Thobias Adengenye alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi majira ya saa 9 alasiri katika kijiji cha Sinya Vilima Saba mpakani mwa Kenya na Tanzania katika njia za panya.

Andengenye alisema polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori walifanikiwa kukamata watu hao wakiwa na mifuko 50 ikiwa na bangi ndani gari hilo mali ya Zephania Kambei mkazi wa Ngaramtoni mkoani Arusha.

Alisema dawa hizo zilikuwa zikisafirishwa kutoka vijiji vilivyo kando kando ya mlima Meru kuelekea Nairobi nchini Kenya kupitia njia isiyo rasmi maarufu kwa `njia ya panya’ iliyopo huko Sinya vilima saba.

No comments:

Post a Comment