Saturday, May 26, 2012

mwanamke akamatwa na pikipiki tano za uizi




JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa sugu 90 wa uhalifu, akiwamo mwanamke ambaye alikutwa na pikipiki tano za wizi pamoja na marobota 145 ya nguo za mitumba.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema katika tukio la kwanza, Mei, 22 mwaka huu katika maeneo ya Ubungo Kibo polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wasamaria wema walifanikiwa kukamata pikipiki tano za aina mbalimbali.


Mbali na pikipiki hizo pia walifanikiwa kukamata vibali vya bima vipatavyo 20, kofia ngumu za pikipiki 10, tangi za mafuta ya pikipiki 6, funguo za pikipiki 20, namba za usajili 8 na spea mbalimbali za pikipiki.


Aidha jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa Shatui Tarimo ambaye ni mama wa nyumbani.


Pikipiki zilizokamatwa ni zenye namba T853 BWT aina ya T-Better, T407 BKY Falcon, T987 BWD, T660 BQQ T-Better ambazo zote ni mali ya wizi. Katika tukio jingine, Kova alisema Mei 17, mwaka huu baada ya kupokea taarifa kutoka kwa wananchi katika maeneo ya Vingunguti kwa Simba walifanikiwa kukamata marobota 145 ya nguo za mitumba.


Tukio hilo lilifanikiwa baada ya polisi kufanyia kazi taarifa hizo ambapo mzigo huo ulikutwa katika gari aina ya Fuso lenye namba T230 BDR.


Watuhumiwa waliokamatwa katika tukio hilo ni dereva wa gari hilo Gaston Nsagabe na Nelson Kiwelo ambaye ni utingo na wote wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.


Wakati huo huo, Kova alisema wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sugu 90 wa uhalifu katika maeneo mbalimbali ya jiji hili, kwa tuhuma mbalimbali zikiwemo za wizi wa kutumia nguvu wa garini, ukahaba, kubughudhi abiria na makosa mengine.




No comments:

Post a Comment