Friday, June 1, 2012

Nanyaro ahimiza nidhamu Jeshi la Magereza

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali Augustino Nanyaro
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali Augustino Nanyaro, amewataka askari  magereza nchini wawe na nidhamu katika kazi ili kulinda heshima ya jeshi hilo ndani na nje ya nchi.

Aliyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwavisha nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Nne maafisa na Askari magereza 70 wa kanda ya mashariki inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi.


Wengine ni kutoka kikosi maalum cha kutuliza ghasia Magereza, Chuo maafisa Magereza Ukonga na Bohari Kuu ya Magereza Keko, ambao awali hawakuvishwa nishani hiyo na Amiri Jeshi Mkuu,  Rais Jakaya Kikwete.


Nanyaro aliwataka Askari hao wawe na nidhani na utii katika kazi pamoja na askari wengine ambao hawajatunukiwa nishani hiyo.


Katika sherehe hizo zilizofanyika katika viwanja vya Chuo cha Magereza Ukonga, askari magereza 61 walitunukiwa nishani hiyo na wengine tisa hawakuwepo kutokana na udhuru.



No comments:

Post a Comment