Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya
Mrisho Kikwete akifungua mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB)
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr.
Alassane Ouattara (kushoto) akibadilishana mawazo na Rais wa wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr.Donald Kaberuka(kulia) wakati wa sherehe za
ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika
Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Ivory Cost Dr.
Alassane Ouattara akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika
Rais wa wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Dr.Donald Kaberuka akihutubia wakati wa sherehe za ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Jakaya
Mrisho Kikwete(kulia) akibadilishana mawazo na Waziri wa Fedha Dr. William
Mgimwa (kushoto) wakati wa sherehe za
ufunguzi wa mkutano wa 47 wa mwaka wa
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa 47 wa mwaka wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AFDB) wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais
Kikwete wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana mjini Arusha
muonekano wa jengo la mikutano la AICC kwa mbele
Nchi za
Afrika zinarasilimali nyingi lakini baadhi zimeshindwa kuendelea kutokana
na kutokuwa na mfumo mzuri wa usimamizi wa rasilimali hizo ili kuondokana na
tatizo la umaskini.
Hayo yalisemwa leo Jijini Arusha na Rais Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akifunga mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB)ulioshirikisha wajumbe zaidi ya 2000 kutoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika pamoja na Ulaya.
Alisema Afrika inafursa nzuri ya uwekezaji katika sekta ya utalii,kilimo,afya lakini baadhi ya nchi ndio zinanufaika na maendleo hayo kutokana na kusimamia rasilimali zao vizuri pamoja na kuwa na mifumo bora ya utawala pamoja na usimamia wa sheria.
Alisema nchi za kiafrika zinakabiliwa na changamoto kubwa katika kukuza uchumi wake kwa sababu ya hali ya kiuchumi ya kidunia sambamba na swala la chakula pamoja na upandaji wa bei ya mafuta hivyo kupelekea ukuaji wa uchumi kusuasua.
Alisema sambamba na changamaoto hiyo pia tatizo la teknolojia ndio linazozirudisha nyuma nchi za kiafrika kwa maana teknilojia kubwa ambazo nchi za kiafrika zinategeamea nyingi zinatoka nchi za nje.
Aidha raisi Kikwete ametoa rai kwa nchi za kiafrika katika kuondokana na changamoto hizo ambazo zinarudisha nyuma uchumi wa Afrika badala yake aliwasihi waafrika kuchangamkia fursa zilizopo katika nchi zao
ambazo wakizitumia ipasavyo uhakika wa maendeleo utakuwepo.
Miongoni mwa fursa zilizopo Afrika ni pamoja na rasilimali za utalii endapo kama watatumia rsilimali ya utalii ambapo zaidi ya nusu ya watalii duniani hufanya utalii wao katika nchi za kiafrika na kuingiza pato kubwa kwa taifa .
Sambamba na kuangalia sekta hiyo ya utalii pia Kikwee alisema kuna umuhimu mkubwa sana wa nchi za kiafrika kuangalia na kuweka mazingira mazuri ambayo yatawavuti watalii kwa wingi ikiwemo kuweka miundombinu
bora ya Barabara, Viwanja vya ndege pamoja na bandari zetu.
Aliongeza kuwa endapo mazingira ya miundo mbinu yataboreshwa sekta ya utalii Barani Afrika itaingiza pato kubwa akitolea mfano nchi ya Tanzania kwa kusema kuwa kwa sasa pato kubwa linatoka katika madini na
huku utalii ikiwa inashika nafasi ya pili kwa kuingiza pato kubwa.
Faida ambayo nchi za kiafrika zitaiata kwa kukuza utalii ni kubwa kwa sababu katika sekta hii watalii wanapokuja huleta mafanikio ndani ya nchi husika tofauti na sekta ya madini ambapo wanaochimba huja kuchimaba na kuondoka nayo madini.
Naye Rais wa Benki ya AfDB,Dk, Donald Kaberuka Alisema AfDB inatoa misaada kwa nchi mbalimbali na kusisitiza kuwa misaada hiyo ilenge kuwasaidia wahusika pamoja na kuziinua taasisi ndogo ambazo zinahitaji misaada ya kifedha kwaajili ya kuendelea biashara zao pamoja na kutoa angalizo kwa Afrika kusimamia haki, sheria na utawala bora ili kila nchi iweze kunufaika na rasilimali zake.
Naye Rais wa Ivory Cost, Alassane Ouattara alisema nchi hiyo ilikumbwa na machafuko ya kisiasa lakini hivi sasa hali ya serikali imejitahidi kumaliza suala hiyo na amani imerudi tena.

No comments:
Post a Comment