Serikali
imetakiwa kuchukua hatua za haraka kukabiliana na mfumuko wa bei uliopo
kama ilivyoagizwa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC-CCM).
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya CCM, Amina Makilagi, alisema umoja huo unapongeza uamuzi huo wa Nec.
Makilagi alisema mbali na serikali kuchukua hatua za haraka lakini pia
iendelee na mipango yake ya muda mrefu ya kukabilia na tatizo hilo la mfumuko wa bei za bidhaa hasa za vyakula.
Alifafanua kuwa maamuzi ya NEC kuiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka na muda mfupi ikiwamo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula na ya ongezeko la thamani (VAT) katika sukari itasaidia kupunguza mfumuko wa bei na kuwaondolea mzigo wa gharama za maisha Watanzania.
Aliiomba Serikali kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni hasa katika hoteli na maduka mengine yanayotoa huduma kwa wananchi na kuwahimiza waajiri wahimizwe kupandisha mishahara na malipo mengineyo kwa wafanyakazi.

CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment