![]() |
Pichani mtoto Neema George aliyegundulika kuwa na matundu matatu kwenye moyo. |
Mtoto Neema George (16) amewaomba wasamaria wema wajitokeze kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.
![]() |
Miguu ya Neema |
Hali
ya Neema George inazidi kuzorota siku baada ya siku, miguu ikiwa
imevimba, akitaabika katika suala la kula, kuongea na akipata maumivu
makali ya tumbo hasa nyakati za usiku.

Baba
mzazi wa Neema, George Mugunga (kushoto) anasema kuwa mnamo mwaka 2010
mara baada ya hali ya mtoto wake kuzorota alimfikisha katika hospitali
ya Rufaa Bugando kwaajili ya matibabu, lakini mara baada ya vipimo
kufanyika vikaonyesha kuwa moyo wa mtoto wake una matundu matatu.
![]() |
Baadhi ya vithibitisho vya tiba. |
Madaktari
kupitia kliniki aliyokuwa akipata huduma (Bugando) wamesema kuwa
tatizo la neema ni kubwa na haliwezi kupatiwa ufumbuzi hapa nchini bali
linaweza kupata tiba Nchini India kwa makadirio ya gharama ya shilingi
za kitanzania milioni 25.
![]() |
Picha
za ukutani wakati wa ubatizo wa Neema, katika kipindi hicho ingawa
hali yake ilikuwa dhoofu lakini suala la kuvimba tumbo na miguu
halikuwepo.
|
Mbali
na kumtegemea mungu kwa kila azungumzalo mtoto huyu anaonekana
anaakili sana na mwenye uchangamfu wa ndani tatizo linabaki kuwa
anaumwa.
![]() |
Neema akiwa na mwandishi wa habari hizi Albert G. Sengo aliyefika nyumbani kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza kwaajili ya kuchukuwa taarifa zaidi. |
Kutokana
na kiwango kilichotamkwa kuwa kinahitajika kwa ajili ya tiba nje ya
nchi, familia ya mtoto huyu ilikata tamaa kabisa na kukata shauri la
kumpeleka Sengerema kijijini ili akatibiwe na waganga wa kienyeji ndipo
bwana Azizi Bukene (ambaye ni jirani yao) akashauri kuita vyombo vya
habari kwaajili ya kulifikisha kwa umma kwa msaada.
![]() |
Nje ya nyumba. |

Familia
ya mtoto huyu inategemea kilimo kama sehemu ya kipato cha kuendesha
maisha ya kila siku, hivyo uwezo wa kufikisha kiwango hicho cha fedha
hata kupata matibabu kwa manufaa ya mtoto huyo kuendelee na masomo ni
ndoto za alinacha.
No comments:
Post a Comment