Freeman Mbowe
Willbroad Slaa kutofautiana.
Hali hiyo ilisababisha msuguano mkali ndani ya kikao cha ndani cha tathmini kilichofanyika mjini Ruangwa muda mfupi baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi
Likangara mjini hapa.
Kutibuana huko kulitokana na Mbowe kukataa mpango wa Dk. Slaa kutimua viongozi katika maeneo mbalimbali ambako ziara hiyo imefanyika wakiwemo viongozi karibu wote wa wilaya Ruangwa mkoani Lindi.
Kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Chama cha Walimu (CWT) wilayani Ruangwa, ambapo Mbowe alipinga hatua ya Dk. Slaa kutaka baadhi ya viongozi akiwemo Mwenyekiti wa Wilaya Abdallah Mang'onyola na mlezi wa chama hicho wilayani hapa Juma Lichonyo ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho waachie madaraka.
Kikao hicho kilichoanza majira ya saa 2: 30 usiku hadi saa tano, kilifanyika baada ya kumalizika kwa mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali na kupata mafanikio kidogo.
Habari za ndani za uhakika zinasema kuwa mahudhurio hafifu ya watu ndiyo yamemsukima Dk. Slaa kuamuru kufukuzwa kwa baadhi ya viongozi hao akidai wamekisaliti chama hali iliyomfanya Mbowe kupinga, akisema
mpango huo unasababisha chama kulegalega.
Kwa mujibu taarifa za uhakika mkutao huo ulilenga kufanya thathmini baada ya ziara ya viongozi wa Chadema wilayani hapa kukosa watu wengi katika mikutano yao tofauti na matarajio yao hivyo kudai ni hujuma zinafanywa na
viongozi waliowatimua.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment