MABALOZI
wapya walioapishwa jana wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza
ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.Naimi Asizi
(Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda), Dora Msechu (Mkrugenzi wa
Idara ya Ulaya na Amerika), Ramadhan Mwinyi (Naibu balozi wa kudumu
katika Umoja wa Mataifa) na Irene Kasyanja (Mkurugenzi kitengo cha
Sheria).
Wengine ni Vicent Kibwana (Mkurugenzi Idara ya Afrika),
Celestin Mushy (Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa), Hassan
Yahya (Mkurugenzi wa Mashariki ya Kati), Silima Kombo Haji (Mkurugenzi
wa Mambo ya nje Zanzibar) na Mbelwa Kairuki (Mkurugenzi wa Asia na
Australia).
Akizungumza baada ya hafla hiyo, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alisema hadi sasa kuna
mabaliozi 32 walioko nje ya nchi na kwamba sasa wamefikia 42 na kwamba
wamezingatia jinsia, umri na muungano katika kuteua mabalozi hao.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti mara baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete
jana, mabalozi hao waliahidi kufanya kazi kwa ushirikiano.
Mmoja
wa mabalozi hao, Naimi Asizi aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Idara ya
Ushirikiano wa Kikanda, alisema atahakikisha Tanzania inafanya vizuri
katika Jumuiya mbalimbali kama za Afrika Mashariki, soko la pamoja
(Comesa) na SADC.
Naye Balozi Dora Msechu alisema kuwa kuna
changamoto nyingi za kukabiliana nazo kwa sasa hasa katika jumuiya
mbalimbali hivyo atajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili kukuza
ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.
Naye balozi
Bertha Somi ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Watanzania
wanaoishi ughaibuni, alisema atafanya kazi kwa bidii na kuhakikisha
Watanzania wanaoishi nje wanachangia maendeleo ya nchi.
|
|
No comments:
Post a Comment