habari na pual joseph manyara
Wananchi
wa Wilaya ya Mbulu wameandamana hadi katika ofisi ya Mkuu wa wilaya
kupinga kitendo cha kufungwa kwa ofisi ya serekali na kiongozi kufanya
shughuli ya kuendesha pikipiki maarufu kama boda boda badala ya
kuhudumia wananchi kama alivyo agizwa na serekali.
Wakiongea
kwa jazba mbele ya Mkuu wa wilaya Bw Anator Choya wananchi wamebainisha
kuwa ofisa mtendaji wa kata Ayamamii Bw Ibrahimu Tsere amekuwa amekuwa
akifunga ofisi ya kijiji hivyo kuwawiya vigumu kupata huduma za serekali
na kila wanapojaribu kumuuliza kuhusu swala hilo amekuwa akiwatolea
vitisho.
Mkuu wa wilaya Bw Choya aliagiza mtendaji huyo
afikishwe mara moja kwenye ofisi ya wilaya ili aeleze sababu ya kufunga
ofisi na kufanya mambo ambayo ayahusiani na kazi ya serekali kwani
kuendesha boda boda ni shughuli yake binafsi isiyo na manufaa kwa
wananchi, `Kesho asubuhi naomba mkurugenzi wa halmashauri ya Mbulu aje
na mtendaji huyo hapa ofisini ili atueleze kazi aliyo tumwa na serekali
laasivyo pikipiki yake tutaichukuwa na kama asipo kuja kwa hiyari polisi
watamchukuwa wamlete hapa` alisema Bw Choya.
Aidha mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw Simoni Mayeye alisema kwa upande wa
wananchi ni halali kupata huduma za afisa mtendaji na hata atua
waliochukua ni sawa kwani hili ni swala la msingi kwa wananchi`
Maandamano haya ni ushahidi tosha kuhusu kufungwa kwa ofisi na mtendaji
huyo na sisi tumesha toa maagizo kuwa ofisi za serekali zifanye kazi kwa
muda wote na hapa lazima hatua za kinizamu zichkuliwe juu ya mtendaji
huyo` Alisema Bw Mayeye
Wananchi walimchagua Bw John Darabe
kuwa katibu wa kata katika kikao kilicho amriwa na mkuu wa wilaya
kufanyika kwa lengo la kutatua tatizo la uongozi wa kijiji hicho mkutano
ambao mkuu wa wilaya amewaahidi wananchi kuwa kero zao zote
zitasikilizwa na kutatuliwa.
Mmoja kati ya wananchi hao Bw
Israeli Bilauri alibainisha kuwa wamekuwa wakinyanyasika na vitisho vya
mtendaji huyo na wamekuwa wakikosa huduma za serekali, `Ofisi hii
imekuwa ikifunguliwa siku anayo take yeye mwenyewe na tulipo jaribu
uliza alitujubu kuwa sisi hatuku mwajiri yeye nay eye ndinye mwenye
maamunzi` alisema Bilauri.
Vitendo vya viongozi wa serekali za
vijiji na kata kuwazarau na kuwapuuzia wananchi vimekuwa vikijitokeza
hasa katika maeneo ya vijijini na kuwakosesha wananchi haki zao za
msingi kwani viongozi hawa wamekuwa kama wafalme katika jamii kwani hata
wakifanya maamuzi wanafanya kwa manufaa yao binafsi na wananchi hawana
cha kufanya Bwana Israel Bilauri aliweka wazi kuwa Mzee Margwe Masang
kuchukuliwa dume la ng`ombe na uongozi wa kijiji kwa kushindwa kutoa
mchango wa elfu sitini na tano (65) na wamekuwa wakimzungusha Mzee huyo
mapaka leo ` Huyo ni Mzee na imewekwa wazi kuwa wazee hawatakiwi
kuchangia lakini kwanini mambo haya lakini kwanini wamemchukulia dume la
ng`ombe na sasa kumlipa mzee huyo ng`ombe wake uongozi unamzungusha
tuu mpaka leo` alisema Bilauri
Wakati huo huo
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Genda wilayani Mbulu mkoani Manyara (
20) amanusurika kubakwa na watu wawili wakati akitoka katika masomo ya
jioni.
Pascalina ameeleza kuwa akiwa anatoka kujisomea darasani
alikutana na watu wawili wakamwomba awaonyeshe njia na ndipo alipo
sogea karibu wakamshika na kumpeleka katika uwanja wa mpira Sanu na
kumuekea nguo mdomoni na kuanza jaribio la kumbaka lakini alijitahidi
kupambana na wabakaji na alifanikiwa kutoroka kutoka katika mikono ya
wabakaji hao
Vitendo vya ubakaji kwa sasa vimeshamiri katika
mkoa wa manyara na jamii inekuwa ikihofia kutoa taarifa kwa jeshi la
polisi kwa kuhofia kutoa ushahidi mahakamani kwani mara tuu baada ya
jaribiao hilo wahalifu hao walikimbila kusiko julikana Mlezi wa
Pascalina Bi Maria Naasa alisema kuwa `Ningumu kwa sasa kupeleka swala
hili polisi kwani Pascalina ni mgeni hapa na hata wahalifu hao hawajui
akiwaona sasa kweli swala hili utawaambiaje polisi nay eye hawajui
wabakaji`
Wakazi wa Sanu wameeleza kuwa matukio ya ubakaji na
wizi yameshamiri kwa kasi katika maeneo yao na hasa katika eneo la
Uwanja wa Mpira kwani hili ni moja tuu kati ya matukio mengi yanayo
tokea eneohilo na jamii imekaa kimya kwani kumesha wahi kutokea ubakaji
mwingine katika eneo hili.
Bwana Herman Kita ni mkazi wa Sanu
alibainisha kuwa waalifu wanaotenda vitendi hivyo wanajulikana, `
Wabakaji wanajulikana tatizo ni wazazi wao ni watu wenye pesa sasa na
wamekuwa wakifanya ubakaji katika eneo la uwanja wa mpira lakina hakuana
cha kuwafanya wazaziwao wanauwezo kipesa sasa kila siku unasikia binti
wa flani kabakwa na watoto wa mzee flani sasa hatuna chakufanya na hata
kama tukienda polisi kesho wanatoka` —
No comments:
Post a Comment