JESHI la
polisi mkoani hapa limefanikiwa kukamata pombe lita 9000 ya pombe haramu aina
ya gongo iliyokuwa ikisafirishwa kutoka nchini Kenya kuingia nchini Tanzania.
Kamanda wa
polisi mkoani hapa, ACP Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo limetokea juni
10 mwaka huu majira ya saa 12;00 jioni katika eneo la Namanga wilayani Longido,
ambapo askari wa jeshi la polisi mkoani Arusha walifanikiwa kumkamata mtu
mmoja aitwaye Nicolaus Thobias (35) mkazi wa Arusha mjini.
Alisema kuwa
,dereva huyo alikuwa amehifadhi pombe hiyo kwenye pipa 150 ambapo polisi walifanikiwa
kukamata baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema .
Sabas
alisema kuwa, dereva huyo alikuwa amebeba pombe hiyo kwenye gari aina ya Scania
lenye namba za usajili T 416 AJX ambalo linamilikiwa na Joseph Michael Massawe.
Awali baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo,
alisema kuwa anasafirisha spirit lakini mara baada ya upekuzi ikagundulika kuwa
ni pombe haramu ya gongo.
Kamanda
Sabas aliongeza kuwa, kufuatia tukio hilo jeshi la polisi linaendelea
kumshikilia dereva huyo kwa mahojiano zaidi na pindi uchunguzi utakapokamilika
atafikishwa mahakamani kujibu shitaka hiyo.
No comments:
Post a Comment