Saturday, June 16, 2012

Urusi yapinga vikwazo dhidi ya mafuta ya Iran

Urusi leo imepinga  Iran kuwekewa vikwazo kwenye uuzaji wa mafuta yake ikiwa ni siku kadhaa kabla ya kufanyika mazungumzo ya mpango wa nyuklia wa nchi hiyo yatakayofanyika mjini Moscow.

Naibu Waziri wa Mambo ya Kigeni Sergei Ryabkov amesema kuwa ni muhimu kwa Marekani na Umoja wa Ulaya kuachana na mpango wakuiwekea vikwazo vya kiuchumi Iran.


Umoja wa Ulaya umetangaza kuiwekea vikwazo Iran kwenye biashara ya mafuta yake kuanzia mwezi Julai mwaka huu, kama hakutakuwa na maendeleo  kwenye awamu ijayo ya mazungumzo baina ya nchi hiyo na mataifa yenye nguvu duniani kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye utata.

 Ryabkov amesema kuwa Iran inaweza kukutaa kukaa kwenye meza ya mazungumzo siku zijazo kama vikwazo zaidi vitaendelea kuwekwa dhidi yake.  

No comments:

Post a Comment