Saturday, June 16, 2012

Viongozi wa Umoja wa ulaya kuzumgumza kabla ya mkutano wa G20

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatarajia kufanya mkutano kwa njia ya video leo kuujadili mzozo wa uchumi unaozikabili nchi zao ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa kilele wa nchi za kundi la G 20 

utakaofanyika nchini Mexico. Mkutano huo utawahusisha viongozi kutoka Ujerumani, Italia, Uhispania, Ufaransa, Uingereza pamoja na Rais wa Umoja wa Ulaya Jose  Manuel Barroso. 


Msemaji wa Waziri Mkuu wa Uingereza atakayeshiriki kwenye mkutano huo amesema kuwa mazungumzo hayo ni sehemu ya mpango wao wa kawaida waliouweka kuelekea mkutano wa G20. 

 Mkutano wa G20 unatarajiwa kugubikwa na mada za mzozo wa uchumi unaozikabili nchi za ulaya pamoja uchaguzi wa Ugiriki.  

No comments:

Post a Comment