Saturday, June 16, 2012

Al-Shabab wajisalimisha

Kundi la wanamgambo nchini Somalia lenye uhusiano na Al-Qaeda ,Al-Shabab, linaonekana kuishiwa nguvu kabisa kwani baadhi ya wanamgambo hao wanaamua kujitoa na kurejea katika maisha ya kawaida. 

Abshiri Ali Mohamed ni miongoni mwa wanamgambo waliokuwa ni tishio katika pembe ya Afrika ambapo ni mafanikio yanatokana na Majeshi ya Afrika kuwafurusha majuma ya hivi karibuni. Hasa katika miji ya Elasha Biyana na Afgoye


Wanamgambo wa Al-Shabab wajitenga zaidi

Mohamed anasema, wanamgambo hao hivi sasa wamejitenga na kundi hilo katika makundi madogo madogo na kuchapuka wengine wamepoteza silaha zao na hawana matumaini. Msemaji wa Serikali ya Somalia Abdirahzman Omar Osman amesema kuwa wanamgambo zaidi ya 500 wa Al-Shabab wamejitenga na kundi hilo na kujiunga na serikali ya taifa hilo na idadi ya wanaoasi inaongezeka kila siku.

Hali hiyo pia inaungwa mkono na Msemaji wa Majeshi ya Umoja wa Afrika Luteni Kanali Paddy Ankunda anaunga mkono kuwa Al-Shabab wamepoteza muelekeo kabisa na hakuna matumaini ya kuibuka tena.
Wanamgambo wa Al-Shabab Wanamgambo wa Al-Shabab
Maoni ya makamanda wa majeshi ya Afrika

Mwezi uliopita Majeshi hayo ya Umoja wa Afrika yaliweza kuwauwa wanamgambo zaidi ya 60 katika mapigano yaliyodumu kwa siku tatu na kufanikiwa kufika Mogadishu kwa mara kwanza tangu mwaka 2007 walipouteka mji wa Mogadishu.

Kamanda wa Majeshi ya Burundi aliyepo katika uwanja wa mapambano Luteni kanali Gregory Ndikumazambo anasema kuwa wanamgambao wa Al-Shabab wanapigana vizuri lakini changamoto kubwa kwa wanamgambo hao hawana mbinu nzuri za mawasiliano ndilo tatizo lao ambalo limefanya majeshi ya Umoja wa Afrika kuwazidi nguvu kwa urahisi.

Haifahamiki uimara wa kundi hilo lakini Mohamedi ambaye alikuwa miongoni mwa askari hao anasema kundi hilo lilikuwa na wapiganaji kati ya 7000-8000 lakini mpiganaji mwingine wa zamani anasema wapiganaji hao ni kati 4000 -6000. Mpaka sasa majeshi ya Umoja wa Afrika yana kikosi askari zaidi ya 17,000 ndani ya Somalia pekee.

Wanamgambo hao walikuwa wakikusanya ushuru katika bandari ya Kisamayuu,bandari katika bahari ya Hindi huku ukiwa ni mji wa biashara wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Lakini kwa upande wake Sheik Mustaf miongoni mwa makamanda wa kundi hilo aliwahitaji wale wote wa naokimbia kurejea katika mapambano katika katika mawasilaino ya simu ya mkononi.
Kamnada huyo alimwambia Mohamed kwamba kwani asimreje Allah lakini Mohammed akasema kuwa kuna siku ataualika mkuu wake wa mapabano upande wa Serikali ya Somali.

Wameamua kutunza familia zao

Mohamed Abdi abdullahi akiwa na umri wa miaka 45 ni mpiganaji wa zamani wa Alshabab alijiunga na Al-Qaida na Alshabab kwa mpiganaji wao anasema kuwa hivi sasa nataka kuishi kwa amani na kuitunza familia yake ya watoto watano.

Taifa la Somalia halina amani tangu mwaka 1991 baada ya kuondolewa madarakani kwa kiongozi wa taifa hilo Mohamed Siad Barre ambapo makundi ya wanamgambo ya Kiislamu yakaanza kumiliki baadhi ya maeneo ya taifa hilo na kuingia katika migogoro ya muda mrefu mpaka sasa

No comments:

Post a Comment