Friday, June 15, 2012

Ushindi wa ubunge wa Mnyika mahakamani ‘wakatiwa rufaa’

John Mnyika
Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Ubungo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hawa Ng’humbi, amewasilisha hati ya kusudio la kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, akipinga hukumu ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliyotupilia mbali kesi yake ya uchaguzi.

Kesi hiyo ilikuwa ikipinga ubunge wa Mbunge wa Jimbo hilo, John Mnyika (Chadema).


Ng’humbi aliwasilisha kusudio hilo katika mahakama hiyo jana kupitia wakili wake, Issa Maige, kwa njia ya maandishi.

Alichukua hatua hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Upendo Msuya, kutupilia mbali kesi hiyo namba 107 ya mwaka 2010.

Hukumu hiyo ilitolewa na jaji huyo kwa maelezo kwamba, Ng’humbi alishindwa kupeleka mahakamani ushahidi wa kuthibitisha madai yake.

Katika kesi hiyo, Ng’humbi aliiomba mahakama itamke kwamba, uchaguzi katika jimbo hilo ulikuwa ni batili kwa sababu haukuwa huru na haki na kwamba, taratibu za uchaguzi zilikiukwa.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment