WAMILIKI wa Maduka ya dawa baridi, wametahadhrishwa
kutokuchukua dawa katika hospital za serikali na kuzipeleka kenye maduka yao kwa ajili ya biashara huku hospital zikiwa
hazina dawa kwa ajili ya wagonjwa.
Hayo yameelezwa jana na mganga mkuu wa mkoa wa Arusha, dakta
Frida Mokiti, alipokuwa akifungua mafunzo ya wiki moja ya watoa dawa katika maduka ya dawa muhimu, inayoshirikisha
wauzaji wa dawa kutoka halamashauri ya Jiji la Arusha na wilaya ya Arusha
DC,katika ukumbi wa chuo cha Ufundi, Arusha yaliyoandaliwa na mamlaka ya
Chakula na dawa..
Dakta, Mokiti, alisema kuwa kuna baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa
ambao wamekuwa wakitumia ujanja kujipatia dawa hizo kutoka katika hosipital za
serikalini na kuzipeleka kwenye maduka yao
huku wagonjwa wakibakia bila dawa hivyo akawaonya kuacha tabia hiyo mara moja
kwani msako utapita na atakaepatikana akiuza dawa hizo atakabiliwa na wakati
mgumu.
Alisema lengo la serikali kutoa mafunzo hayo kwa watoa dawa katika maduka ya
dawa muhimu, ni ili kuwawezesha kupata elimu bora ya utoaji sahihi wa dawa na
hivyo kuweza kuondoa tatizo huduma hafifu mkoani Arusha.
Alisema mafunzo hayo ambayo yanalenga katika sheria na
kanuni zinazosimamia dawa sanjari na magonjwa yatokeayo mara kwa mara ,matibabu
ya magonjwa ya watoto kwa uwiano ,elimu
ya ukimwi na ushauri nasaha ,mbinu
mbalimbali za mawasiliano na elimu ya uzazi
wa mpango.
Dakta mokiti, alisema kuwa mafunzo hayo ni ya msingi na yatawasaidia kuwa watoa huduma wazuri na kuimarisha
utendaji wao ,na dawa zitatumika kwa usahihi
na kutoa matunda yaliyokusudiwa na madaktari ,pia wakumbuke kuwa dawa ni
sumu iwapo hazitatumika ilivyokusudiwa
zinaweza kulata madhara ambayo
hayakutarajiwa kwa watumiaji.
Awali Meneja wa kanda ya kaskazini Damas Matiko, kutoka
mamlaka ya Chakula na dawa TFDA ,alisema kuwa mamlaka imeaandaa mafunzo hayo
kutokana na tathimini iliyofanywa mijini na vijijini, na kubaini kuwepo kwa matatizoya upatikanaji
wa huduma za msingi imeendelea kuwa ni tatizo
katika sekta hiyo ya dawa baridi hivyo mafunzo hayo yatasaidia kupata
ufumbuzi wake.
Alisema katika tathimini hiyo matatizo yaliyojitokeza ni
pamoja na watoaji wa dawa katika maduka kutokuwa na elimu ya dawa au tiba ,kuuza dawa moto ambazo
hazikusajiliwa kutoa huduma za tiba kwenye maduka sanjari na kuchoma sindano
wagonjwa na ,kufunga vidonda .
Matiko,alisema kutokana na matatizo hayo serikali kupitia
wizara ya afya na usitawi wa jamii kwa
kushirikiana na MSH ilibuni mpango wa majaribio, ADDO, ambao umetekelezwa katika
mkoa wa Ruvuma kuanzia February 2002 hadi Julai 2005 .
Ameyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa
upatikanaji wa dawa zenye ubora ,usalama na ufanisi, kuimarika kwa mfumo wa
ukaguzi na usimamizi wa ,kuongezeka kwa ubora wa majengo na kiwango cha usafi
wa majengo na watoa huduma, kuanzishwa na kuimarika kwa utunzaji wa nyaraka na
kumbukumbu na staid za kazi kati ya wagonjwa na watoa huduma.
Matiko,alisema kutokana
na mafanikio hayo serikali imeamua kusambaza mpango huo nchi nzima ambapo
umetekelezwa katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara,Rukwa, Morogoro, Singida,
pwani.lindi, mbeya,Kigoma, dodoma,
Iringa, Mara, Tanga, na Manyara .
Mpango huo pia upo katika hatua ya kutekelezwa katika mikoa
ya Shinyanga, Tabora, Kagera, Kilimanjaro, na kwenye makao ya kanda katika miji
mikubwa ya Arusha, Mwanza na dare s
salaam,
No comments:
Post a Comment