Mchakato wa kuelekea demokrasia nchini Misri ambao tayari
umekumbwa na wahaka ulitumbukizwa katika ghasia siku ya Alhamis baada ya
mahakama ya katiba kubatilisha bunge katika kile kilichoitwa mapinduzi
ya kijeshi.
"Tulifanya mapinduzi na hakuna mapinduzi yoyote duniani yanayorejesha utawala wa kibabe. Baraza la kijeshi linataka kurejesha utawala wa zamani, na wanataka turudi kuwa watumwa. hatutorudi kuwa watumwa, tutaendelea kupambana, na kupambana dhidi ya Ahmed Sahfique, na tutaendelea. Mungu akipenda," alisema Mohammed Hussein.
Uchaguzi kuendelea kama ilivyopangwa
Wamisri wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumamosi na Jumapili katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais ambapo Ahmed Shafique anapambana na mgombea kutoka chama cha Udugu wa Kiislam, Mohammed Mursi. Shafique amabye ni Jenerali wa zamani wa jeshi alikaribisha hukumu hiyo ya mahakama na kuongeza kuwa ulikuwa wa kihistoria.
Kundi la vyama sita vya siasa lilitoa taarifa likisema kuwa Baraza Kuu la kijeshi (SCAF) limedhamiria kurudihsa utawala wa zamani na kwamba uchaguzi unaofanyika mwishoni mwa wiki hii ni geresha tu. Vyama hivyo, kikiwemo cha Uhuru na haki vimemtaka Mgombea wa Udugu wa Kiislam Mohammed Mursi kujiondoa katika kinyanganyiro hicho.
Kundi hilo limewataka pia wabunge wote kujiunga na wanamapinduzi dhidi ya utawala wa kibabe wa majenerali wa kijeshi. Hukumu hii imezidi kuleta mchanganyiko kwa vile hata mamlaka ya rais atakayechaguliwa yalitakiwa kubainishwa na Baraza la katiba ambalo liliteuliwa na Bunge wiki iliyopita.
No comments:
Post a Comment