Wamisri wameanza kupiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa
rais wa nchi hiyo kati ya mgombea anayefuata siasa zinazoegemea dini
ya Kiislamu dhidi ya waziri mkuu wa zamani wa utawala wa taifa hilo.
Ahmed Shafiq, waziri mkuu wa mwisho wa rais alieondolewa madarakani Hosni Mubarak anapambana na mgombea wa chama cha Udugu wa Kiislam, Mohammed Mursi katika zoezi la kupiga kura litakalodumu kwa siku mbili ambapo kiasi ya raia milioni 50 wamejiandikisha kushiriki zoezi hilo.
Vituo vya kupiga kura vilifungulwia mapema leo kote Misri
Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa mapema asubuhi ambapo kiasi ya
askari 150,000 wametawanywa kwa nia ya kudhibiti hali ya usalama
kwenye uchaguzi huo wenye mgawanyiko mkubwa. Kinyang'anyiro hicho
kimeleta mtengano na hasa kwa wale wenye hofu ya kurejea madarakani kwa
uongozi wa zamani kupitia Shafiq na wale wanaotaka kutenga siasa na dini
na shaka kwamba chama cha Udugu wa Kiislamu kitavuruga uhuru wa watu.Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo Mursi alipata asilimia 24.7 ambapo Shafiq ambae pia alikuwa kamanda wa jeshi la anga alipata asilimia 23.6 ya kura.
Uchaguzi huo unakuja huku kukiwa na hali ya vurugu ambalo linaweza kusababisha uongozi wa kijeshi, ambao ulichukua madaraka wakati rais Hosni Mubarak alipojiuzulu Febrauri mwaka jana, inaendelea kuimarisha nguvu zake madarakani.
Alhamis wiki hii, mahakama kuu ya katiba nchini humo ilitoa hukumu kwa baadhi ya vipengee katika sheria inayoongoza uchaguzi wa bunge kuwa ni batili, hii ikiwa ni kulivunja bunge linalodhibitiwa na makundi ya Kiislamu.
Waandamanaji Misri wakipinga umauzi wa kumkubalia Ahmed Shafiq kushuriki uchaguzi
Chama cha ugudu wa Kiislamu kilipata asilimia 47 ya viti
katika hatua ya mpambano kati ya mwezi Novemba mwaka jana na
Februari mwaka huu.Mahakama hiyo ya juu pia imetoa hukumu kuwa sheria inayowatenga baadhi ya wanasiasa kuwa ni kinyume na katiba, sheria ambayo inawazuwia maafisa waandamizi wa utawala wa mubarak pamoja na wanachama wa ngazi ya juu wa chama ambacho hivi sasa kimefutwa kutogomea wadhifa wowote wa uongozi nchini humo kwa muda wa miaka 10. Sheria hiyo , iliyopitishwa na bunge mapema mwaka huu, imetishia kumzuwia Shafiq kugombea uongozi.
Vyama vya siasa nchini Misri pamoja na wanaharakati wamelishutumu baraza kuu la uongozi la majeshi ya ulinzi kwa kufanya mapinduzi, baada ya hatua kadha ambazo zinaimarisha madaraka yake kabla ya uchaguzi. Uamuzi huo wa Alhamis wiki hii umekuja siku moja baada ya uamuzi wa wizara ya sheria kuwapa wanajeshi haki ya kuwakamata raia baada ya uwezo huo kuondolewa wakati sheria ya hali ya hatari iliyodumu kwa muda wa muongo mmoja kumalizika muda wake hapo Mei 31.
No comments:
Post a Comment