Wednesday, June 27, 2012

Watu wawili wauawa kaskazini mwa Mali

Watu wawili wameuwawa nchini Mali baada ya waasi waliojitenga kukabiliana na waandamanaji katika mji wa Gao, kaskazini mwa nchi hiyo.
Watu wengine kadhaa walijeruhiwa wakati wanamgambo wa Tuareg walipoufyetulia risasi umati wa watu mjini humo hapo jana.

 Kwa mujibu wa tovuti za vyombo vya habari nchini Mali, waandamanaji hao walikuwa wakipinga mauaji ya diwani wa eneo hilo yaliyofanywa Jumatatu iliyopita, huku wakiwashutumu waasi wa Tuareg kwa kuhusika na mauaji hayo.
Hali ya wasiwasi imeongezeka mjini Gao tangu waasi wa Tuareg na wanamgambo wa kiislamu walipoungana kuidhibiti miji kadhaa mapema mwezi Aprili mwaka huu.

No comments:

Post a Comment