Wednesday, June 27, 2012

Kuwatahiri wavulana si halali Cologne

Mahakama ya mji wa Cologne magharibi mwa Ujerumani imepitisha kwamba kuwatahiri wavulana wadogo kwa misingi ya kidini si halali.
 Mahakama hiyo imesema kitendo hicho kinasababisha maumivu makali na uharibifu wa mwili hata kama wazazi wameridhia.
 Imepitisha kuwa haki ya mtoto kuwa na mwili kamili aliozaliwa nao ni muhimu zaidi kuliko uhuru wa kidini na haki za wazazi.

 Uamuzi huo unafuatia kesi iliyomkabili daktari mmoja wa Cologne aliyemtahiri kijana wa miaka minne kwa ridhaa ya wazazi wake.
Operesheni aliyoifanya ilisababisha athari za kitabibu kwa kijana huyo. Uamuzi huo umewaghadhabisha Wayahudi na Waislamu ambao kwa kawaida wamekuwa wakiwatahiri watoto wao wa kiume.
Mkuu wa baraza la Wayahudi la Ujerumani amesema uamuzi huo wa mahakama haukutarajiwa na haujali masilahi.
 Ni uamuzi wa kihistoria unaotarajiwa kuweka mfano wa kisheria wakati mahakama zitakapokuwa zikikata kesi kama hizo.

No comments:

Post a Comment