Monday, July 16, 2012

Mageuzi ya nishati Ujerumani

Chama kikuu cha upinzani nchini Ujerumani,SPD kimetoa mwito wa kuanzishwa wakala wa ushauri juu   ya kutekeleza mageuzi ya nishati nchini.
Mwenyekiti wa chama hicho  Sigmar Gabriel amesema  mjini Berlin kwamba madhali serikali imekiri kushindwa  katika jambo hilo, sasa itapaswa ikabidhi jukumu kwa wengine.

Waziri wa mazingira Peter Altmaier alieteuliwa  kuharakisha juhudi za kuleta mageuzi ya nishati amekiri kwamba mipango kabambe ya kuachana na  matumizi ya nishati ya nyuklia, sambamba na kupunguza hewa chafu ya kaboni, huenda  isifanikiwe.


 Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Gabriel ameshauri kuundwa kwa taasisi ya ushauri itakayopaswa kuwajumuisha wawakilishi kutoka sekta za viwanda,uchumi, na jamii. Amesema wawakilishi hao ndio watakaopaswa kutoa mapendekezo kwa wanasiasa. 

No comments:

Post a Comment