Monday, July 16, 2012

Uchaguzi wa bunge wafanyika Congo

Duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge imefanyika  katika Jamhuri ya Congo
. Mwito ulitolewa kwa watu karibu milioni mbili wenye  haki ya kupiga kura wa kuwachagua wajumbe wanaogombea  viti 135 vya bunge.

 Lakini mahojiano na wapiga kura katika mji mkuu, Brazzaville yameonyesha kwamba ushiriki wa wapiga  kura ulikuwa wa kiwango cha chini.
Vyama vya upinzani vimelalamika kwamba havikupewa haki sana katika maandalizi ya kampeni za uchaguzi.

Duru ya pili ya uchaguzi imepangwa kufanyika tarehe  5 ya mwezi ujao .Mpaka sasa chama cha  Rais Sassou  Nguesso, Congolose  Workers' Party  ndicho chenye  viti vingi bungeni kwa pamoja na vyama  vinavyofungamana nacho.


 Vyama vya upinzani kwa  pamoja vina wabunge 12. Inatarajiwa kwamba kambi ya Rais Nguesso itapata kura nyingi ili kuyadumisha mamlaka. 

No comments:

Post a Comment