Monday, July 16, 2012

Viongozi wa Afrika wakutana Addis Ababa

Umoja wa Afrika umesema kuwa upo tayari kupeleka  jeshi la kulinda amani mashariki mwa Jamhuri  ya  Kidemokrasi ya Kongo.
Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo Jean Ping amewaambia viongozi wanaohuduria mkutano wa wa kilele mjini Addis Ababa kwamba Umoja wa Afrika  upo tayari kuchangia katika kuunda jeshi ili   kuzikomesha shughuli  za makundi yenye silaha katika  Jamhuri ya Kidemkrasi ya Kongo.


Kwenye mkutano huo hatua pia zimepigwa kuhusiana  na mgogoro baina ya nchi mbili za Sudan.
 Na habari zaidi ,kutoka Addis Ababa zinasema  uchaguzi wa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Afrika unatarajiwa kutangazwa baadae.
 Waziri wa mambo ya ndani wa Afrika Kusini Nkosazana Dlamini-Zuma anaugombea wadhifa huo  katika kinyang'anyiro na Mwenyekiti wa sasa  Jean   Ping.  

No comments:

Post a Comment