Thursday, July 5, 2012

MEGATRADE YATOA MILIONI 1.5 KWA AJILI YA TAMASHA LA WAANDISHI WA HABARI ARUSHA

 Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Megatrade Gudluck Kway akifafanua jambo katika kikao cha waandishi wa habari kabla ya kukabidhi hundi
Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Megatrade, Gudluck Kway, akimkabidhi Katibu wa TASWA Arusha , Mussa juma, hundi ya sh 1.5 milioni, kama udhamini wa Kampuni hiyo katika bonanza la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini, ambalo litafanyika julai 15 mwaka huu, makabidhiano hayo, yalifanyika palace Hoteli mjini Arusha.
 katibu wa chama cha waandishi wahabari wa michezo Mussa Juma akiwa anaongelea mashindnano hayo



MAKAMPUNI kadhaa, yamejitokeza kudhamini Tamasha la saba la vyombo vya habari kanda ya Kaskazini, ambalo litafanyika Julai 15 katika Viwanja vya General Tyre mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari  Palace Hoteli, Katibu wa Chama cha waandishi wa habari za michezo na Burudani mkoa wa Arusha(TASWA ARUSHA), Mussa Juma alisema   Makampuni ambayo yamekamilisha udhamini wake ni, Kampuni ya Bia nchini(TBL), Kampuni ya simu la Alphatel na Kampuni ya Megatrade Investment(T) Ltd.

Juma alisema  wadhamini wengine ni Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA), Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na mengine kadhaa ambayo yatatangazwa hivi karibuni.

Katibu huyo, alisema katika tamasha la mwaka huu, zawadi mbali mbali zimetengwa kwa wanahabari, ikiwepo vikombe na fedha taslimu, katika kuhamasisha michezo na mahusiano baina ya wanahabari na taasisi nyingine Kanda ya Kaskazini.

Akizungumza wakati akikabidhi hundi ya sh.1.5,Meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Megatrade Investment(T) Ltd, Godluck Kway, alisema kampuni hiyo, imeamua kudhamini bonanza hilo kama ishara ya kutambua jitihada za wanahabari mkoani Arusha.

Kway alisema kampuni hiyo, imejipanga kuhakikisha itachangia masuala ya kijamii, kutokana na sehemu ya faida ambayo wamekuwa wakipata kutokana na kuuza bidhaa zao mbali mbali za vinywaji vikali.

"hii ni mara yetu ya kwanza kusaidia tamasha hili, lakini tunaahidi tutaendelewa kufanya hivi katika miaka ijayo"alisema Kway.

Tamasha hili,ambalo hufanyika kila mwaka, huandaliwa na kampuni ya MS Unique Promotion kwa Kushirikiana na chama cha waandishi wa habari za michezo(TASWA ARUSHA). na litahusisha michezo ya soka, kuvuta kamba, mbio za magunia, kukimbiza kuku na kucheza muziki.

No comments:

Post a Comment