Friday, July 6, 2012

Wikileaks kutoa nyaraka za Syria

Mtandao unaotoa nyaraka za siri wa Wikileaks umetangaza leo kuwa utachapisha zaidi ya barua pepe milioni mbili kutoka kwa wanasiasa, wizara na makampuni nchini Syria kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita iliyopita.

 Katika mkutano wa waandishi wa habari mjini London, Wikileaks ilizitaja kile ilikiita kama Nyaraka za Syria, kama "nakala za kushangaza" kutoka kwa mashirika 680 au majina ya watu, wakiwemo mawaziri wakuu serikalini.
 Nakala hizo ni za kipindi cha kati ya mwezi Agosti mwaka wa 2006 hadi Machi 2012. Nyaraka hizo za siri zitachapishwa katika miezi miwili ijayo kwa ushirikiano na vyombo kadhaa vya habari, likiwemo gazeti la Lebanon la al-Akhbar, Masry al-Youmi la Misri, Associated Press na televisheni ya Ujerumani ya ARD, gazeti la L'Espresso la Italia na mtandao wa Publico.es wa Uhispania.


Katika taarifa, muasisi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange alisema nyaraka hizo ni za aibu siyo tu kwa Syria bali pia wapinzani wake. Aliongeza kuwa zinasaidia siyo tu kulishutumu kundi moja au jingine, bali pia kuelewa maslahi yao, vitendo vyao na mawazo yao.

No comments:

Post a Comment