Friday, July 6, 2012

Tunisia yataka uchunguzi kuhusu kifo cha Arafat

Tunisa imetoa wito kwa mawaziri wa nchi za Kiarabu kukutana na kujadili kifo cha rais wa zamani wa Palestina Yasser Arafat baada ya kuzuka madai mapya kuwa aliuawa.

 Mamlaka ya Palestina yalikubali jana kuufukua mwili wa Arafat baada ya madai mapya kujitokea kuwa alipewa sumu iliyokuwa na mionzi ya madini aina ya polonium, sawa na yale yaliyomuuwa jasusi mmoja wa wa zamani wa Urusi mjini London mwaka wa 2006.

 Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Ahmed Ben Helli amesema kuwa kamati kuu ya Jumuiya hiyo ilipokea ombi leo kutoka kwa mwakilishi wa Tunisia kuitisha mkutano wa mawaziri ili kujadili mazingira ya kifo cha kiongozi marehemu Yasser Arafat.


Ben Helli alisema ombi hilo limewasilishwa kwa wanachama wa jumuiya hiyo kwa mkutano na kuamua jinsi wangependa kulikabili suala hilo kwa ushirikiano na Wapalestina.

No comments:

Post a Comment