Friday, July 6, 2012

Hofu ya usalama kabla ya uchaguzi Libya

Wananchi wa Libya pamoja na waangalizi wa kimataifa wana wasiwasi kuhusu hali ya  usalama huku nchi hiyo ikijiandaa kwa uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia wiki hii ,baada ya miongo minne ya utawala wa kiimla chini ya kiongozi aliyeuawa Muamar Gaddafi.

Msemaji wa serikali ya mpito Nasser al-Manaa ametoa mwito kwa wananchi wote wa Libya kushiriki, kulinda na kujivunia uchaguzi huo ambao ni hatua ya kuelekea kwa taifa imara na lenye maendeleo.

Vyombo vya usalama vimeonya kuwa wafuasi wa utawala wa zamani huenda wakatumia fursa kuvuruga kura hiyo ya kulichagua bunge, ambalo miongoni mwa mengine litapewa jukumu la kuiteua serikali mpya.


Wiki kadhaa kabla ya uchaguzi huo, kumezuka ghasia baina ya tabaka za jamii mbalimbali, huku machafuko ya umwagaji damu yaliyotokea katika miji ya eneo la milima la Magharibi yakisababisha vifo vya watu zaidi ya 100. Pia mapigano mapya katika eneo la Kufra, upande wa Kusini yalisababisha vifo vya watu kadhaa.

No comments:

Post a Comment