Friday, July 6, 2012

Ajali ya Fukushima ilisababishwa na kosa la binadamu

Ajali iliyotokea mwaka jana  katika kinu cha nyuklia cha Fukushima ni janga lililosababishwa na makosa ya binadamu na sio tu wimbi la tsunami lililokipiga kiwanda hicho, Ripoti ya mwisho kuhusu mkasa huo iliyotolewa na jopo la wabunge la Japan, imesema kuwa ajali ya kiwanda cha nyuklia cha TEPCO Fukushima, ilitokana na njama ya serikali, shirika la kudhibiti nishati ya nyuklia na mhudumu wa kiwanda hicho, pamoja na ukosefu wa uongozi.

Ripoti hiyo inasema watu hao wote waliisaliti haki ya nchi hiyo ya kuwa salama kutokana na ajali za nyuklia. Wakati huo huo kinu cha kwanza cha nyuklia nchini humo kimeanza kazi tena leo baada ya kusita tangu tetemeko la ardhi la mwaka jana.


 Japan ilifunga vinu vyake vyote, kimoja baada ya kingine, kufuatia mkasa huo, na kuwa bila ya nishati ya nyuklia kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1970. Kinu hicho cha Ohi, Magharibi mwa Japan, kilianza tena kutengeneza umeme kabla ya kutolewa ripoti ya bunge kuhusu ajali ya kinu cha Fukushima.

No comments:

Post a Comment