Mkutano wa kile kinachojulikana kama Marafiki wa Syria ambao
umefanyika katika mji mkuu wa Ufaransa leo, umetaka kuwepo kwa
azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo litaungana
na vikwazo kuishinikiza serikali ya Rais Bashar al Assad kuukubali
mpango wa kuwa na kipindi cha mpito.
Mkutano huo unataka azimio lenye kuzingatia kipengele namba 7 cha mkataba wa Umoja wa Mataifa, ambacho kinaweka uwezekano wa shinikizo la kidiplomasia bila kuruhusu matumizi ya nguvu za kijeshi.
Hata hivyo kipengele hicho kinaposhindwa kutimiza haja, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaweza kupitisha kipengele namba 42 cha mkataba huo ambacho kinaidhinisha matumizi ya nguvu kushurutisha utekelezwaji wa azimio la Umoja wa Mataifa. Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema ili kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria, ukandamizaji wa Rais Assad unapaswa kusimamishwa.
Washiriki wa mkutano huo ambao wametoka nchi na mashirika takribani 100, wameutolea wito Umoja wa Mataifa kutoa mchango wake ili mpango wenye vipengele sita wa mpatanishi wa kimataifa kwa ajili ya Syria, Kofi Annan uweze kuheshimiwa.

No comments:
Post a Comment